Nyumba 62 zilizopo katika Vijiji vya Wilaya ya Kilindi, zimeezuliwa
na nyingine kubomoka kutokana na mvua kubwa iliyoambatana na upepo mkali
kunyesha kwenye maeneo mbalimbali ya Mkoa wa Tanga.
Maafa hayo yamesababisha mtoto mmoja kufa kwa kuangukiwa na nyumba, huku zaidi ya wanavijiji 110 kukosa mahala pa kuishi.
Kwa mujibu wa habari zilizopatikana na kuthibitishwa na Mkuu wa
Wilaya ya Kilindi, Selemani Liwowa ni kuwa nyumba hizo zimeezuliwa usiku
wa kuamkia Ijumaa wiki iliyopita baada ya kunyesha mvua iliyoambatana
na upepo.
Gazeti hili lilijulishwa kuwa mvua kubwa ilinyesha katika vijiji mbalimbali vya wilayani hapa na kusababisha madhara hayo.
Akithibitisha tukio hilo, Liwowa alivitaja vijiji vilivyokumbwa na
maafa hayo kuwa ni Songe, ambako mtoto mmoja amekufa kwa kuangukiwa na
ukuta.
Vijiji vingine ni Kwasetemba, ambako nyumba 16 zimeanguka na Gitu zilikobomoka na kuezuliwa ni nyumba 42.
Alisema ya maafa hayo, Kamati ya Ulinzi na Usalama ya Wilaya Kilindi
iliweza kutembelea kwa lengo la kujionea athari, ambapo hatua inayofuata
ni kutuma wataalamu kutathimini athari na mahitaji kwa waathirika.
0 comments:
Post a Comment