Showing posts with label huzuni. Show all posts
Showing posts with label huzuni. Show all posts

Wednesday, 19 February 2014

Unyama! Kijana Amuua Mama yake kwa Kumpiga na Jembe Kichwani huko KAHAMA..!!

Unyama
Katika hali ya kusikitisha ,kuhuzunisha na isiyokuwa ya kawaida kijana mmoja mkazi wa kijiji cha Mwakuhenga wilayani Kahama mkoani Shinyanga amemuua mama yake kwa kumkata na jembe kichwani na kusababisha kifo chake.
Habari kutoka Kahama zinasema tukio hilo limetokea jana majira ya saa mbili usiku na chanzo halisi cha tukio hilo bado hakijajulikana.

Habari kamili kuhusu tukio hili tutakuletea kupitia kwenye blog hii

Tuesday, 18 February 2014

TUNAOMBA RADHI KWA PICHA HIZI..!!!MKE ACHINJWA NA MUMEWE KISA KUTOMPA UNYUMBA...SOMA ZAIDI MKASA HUU ULIOTOKEA HUKO TABORA

Mkazi mmoja wa Nzega, mkoani Tabora, Juma Kiyabo (45) amemchija mke wake, Wande Monera (34), kabla ya mwenyewe kunusurika kifo baada ya kujijeruhi vibaya shingoni katika jaribio la kutaka kujiua.
Tukio hilo limetokea katika kijiji cha Tazengwa saa 7 usiku wa Februari 16 mwaka huu, huku ikielezwa kuwa sababu ya tukio hilo ni kunyimana unyumba mara kwa mara.

Kaimu Kamanda wa Polisi, ambaye pia ni Mratibu Msaidizi mkoani Tabora, John Kauga amethibitisha kutokea kwa tukio hilo.

Kaunga alisema taarifa za awali zinaonyesha kuwa, mtuhumiwa alikuwa akigombana na mkewe mara kwa mara kwa sababu ya kunyimwa unyumba kabla ya kuamua kuchukua hatua hiyo mbaya.

 Kamanda Kaunga alisema kuwa, mtuhumiwa baada ya kufanya unyama huo, naye alijikata koo kwa lengo la kujiua, lakini hata hivyo jaribio lake lilishindikana na sasa yuko chini ya ulinzi wa polisi.

YAMKUTA MAKUBWA BAADA YA FAKE DIMPOS ALIZOWEKA KUINGIA NDANI NA KUHARIBU NGOZI YA SHAVU,,,,,,JIONEEEEEE MWENYEWEEEEEE HAPA ,,,,,,,,,,,



mwanamke ajulikanaye kama CHERELLE CAMPBELL huko marekani aliyekuwa na mtazamio wa kuwa na madimpoz tangu utoto mwake kwani alikuwa akiyatamani madimpoz ya rafiki yake wa karibu  yalikuwa yakimvutia hata yeye.Hivi karibuni mwanamke huyo aliweza kwenda kufanyiwa upasuaji wa shavu na kuwekewa madimpozi hayo fake ambayo mwanzoni yalikuwa nikama madimpoz ya kawaida yale ya kuzaliwa nayo lakini baada ya mda yalianza kudidimia na kuleta kuaribika ngozi hiyo ya shavu kumfanya haonekane waajabu "nilitumia kama dolla 2500 kufanya surgery ya shavu kwa ajili ya madimpoz lakini sasa ninaonekana vibaya kuliko nilivyo kuwa mwazo".

Mahabusu afariki dunia baada ya KUJINYONGA kwa kutumia tambala la kupigia deki ndani ya choo cha mahabusu ya Kituo cha Polisi..!!

polisi
MAHABUSU, Vumi Elias (30), amefariki dunia baada ya kujinyonga kwa kutumia tambala la kupigia deki ndani ya choo cha mahabusu ya Kituo cha Polisi Tunduma.
 
Elias, mkazi wa Maporomoko-Tunduma, aliyetuhumiwa kwa unyang’anyi wa kutumia nguvu katika eneo la Tunduma wilayani Momba, alifariki dunia jana, saa 12 asubuhi muda mfupi baada ya kufikishwa katika Kituo cha Afya Tunduma kwa matibabu.
 
Kaimu Kamanda wa Polisi mkoani Mbeya, Robert Mayala, alisema Elias aliingia choo cha mahabusu saa 10 alfajiri na kufanya jaribio la kujinyonga kwa kutumia nguo ya kupigia deki.
polisi

Monday, 17 February 2014

HUZUNII HUU..!!! MWANAFUNZI WA MWAKA WA KWANZA AAMUA KIJINYONGA MARA BAADA YA KUFELI MTIHANI




Mwanafunzi wa mwaka wa kwanza wa Chuo cha Ualimu  cha Winneba, nchini Ghana, amejiua kwa kujinyonga mara baada ya jina lake kubandikwa kwenye ubao wa matangazo (notice board) kuwa amefeli masomo matatu.



Jina la mwanafunzi huyo limehifadhiwa kwa sasa, ila inasemwa kuwa sababu ya kujinyoga kwake ni kutokana na kufeli masomo hayo matatu ambapo kungepelekea kufutwa kwake shule hapo.

Sababu hasa ya kifo chake haijajulikana moja kwa moja ila inaaminika ilitokana na hofu ya kutimuliwa chuoni hapo kutokana na kufeli mitihani mitatu.

Wilson Dabuo, ambaye ni muwakilishi wa wanafunzi kwenye baraza la chuo hicho, alieleza kupitia Joy News kwamba chuo hicho kina sheria ya kutimua wanafunzi wanaofeli masomo matatu kwenye mitihani yao.

HUZUNII...HUYU MFUNGWA AOMBA kuahirishwa adhabu ya kunyongwa KWAKE ILI AMPATIE MAMA YAKE FIGO ,AMBAYE NI MGONJWA

Ronaldo Phillips mfungwa anayetarajiwa kunyongwa Marekani
Hukumu ya kunyongwa kwa Ronald Philllips aliyepatikana na hatia ya kumuua mtoto wa miaka mitatu katika jimbo la Ohio nchini Marekan imeahirishwa kutokana na mshitakiwa huyo kuomba kuchangia baadhi ya viungo vyake vya mwili zikiwemo figo ili kunusuru uhai wa mama anayeumwa.

Ronald Phillips alitarajiwa kunyongwa Alhamis kwa njia ya sindano ya sumu baada ya kupatiakana na hatia ya kumuua mtoto wa kike mwenye umri wa miaka mitatu mwaka 1993
 Gavana wa jimbo la Ohio John Kasich amesema kama ombi hilo la mshitakiwa litasaidia kuokoa uhai wa mtu mwingine basi na likubalike, lakini litakuwa jambo geni kuahirishwa kwa adhabu iliyokwisha kupitishwa japo kuwa madaktari wanapaswa kuthibitisha.
Phillips mwenye umri wa miaka 40 alihukumiwa kifo kutokana na makosa ya ubakaji na mauaji ya binti wa rafiki yake wa kike Sheila Marie Evans.

Dawa ya sumu iliyotarajiwa kutumika kumuua Phillips ni aina ya midazolam na hydromorphone, mchanganyiko wa dawa ambayo ingetumika kwa mara ya kwanza nchini Marekani kunyonga watu
Jimbo la Ohio liliamua kutumia mchanganyiko wa dawa hii kwa sababu haikuwa na kiasi cha kutosha cha dawa ya kawaida inayotumika kunyongea watu ijulikanayo kama pentobarbital.

Mama mzazi wa Phillips amekuwa akisumbuliwa na maradhi ya figo na dada yake Phillips pia anasumbuliwa na maradhi ya moyo ambapo anasema anahitaji kutoa viungo vyake haraka iwezekanavyo

Sunday, 16 February 2014

VALENTINE DAY INA VITUKO JAMANI..!!!! MREMBO AFUMANIWA NA MUME WA MTU SIKU YA VALENTINE, APIGWA MPAKA KUZIMIA...


SIMULIZI ya mrembo mmoja ambaye jina lake halikupatikana mara moja inatia majonzi na huzuni lakini habari mbaya zaidi ni kwamba alifumaniwa na mwanaume wa mtu, katikati ya shamrashamra za Sikukuu ya Wapendanao ‘Valentine’s Day’, akapewa kichapo hadi akazimia, Ijumaa Wikienda linakupa zaidi.
Mrembo aliyefumaniwa akipatiwa huduma ya kwanza baada ya kuzimia.
Tukio hilo lililovuta hisia za watu wengi, lilitokea Februari 14, mwaka huu, katika ukumbi mmoja wa ‘kulia bata’ uliopo Temeke jijini Dar es Salaam.
HARUFU YA KASHESHE
Awali, paparazi wetu aliyekuwa akijivinjari ukumbini humo akiwa na njaa ya habari, alimuona dada huyo akiwa na mwanaume mmoja mtanashati wakiwa wamekaa chobingo wakionekana kama vile ni mke na mume halali.
Wakiwa wamejiachia huku wakifurahia sikukuu hiyo ambayo kwa hapa Bongo imegeuzwa maana yake na kufanywa kuwa siku ya ngono, kamera ya Ijumaa Wikienda, iliamua kutulia kwa muda na kuwafuatilia.
 Wawili hao walikuwa kivutio kikubwa miongoni mwa wapendanao waliokuwemo ukumbini humo hasa kwa namna walivyovalia mavazi yao na kupendeza.
Mrembo akiwa amezimia baada ya kipigo.
RANGI NYEKUNDU
Katika kile kilichoonekana mrembo huyo alikuwa amepania sikukuu hiyo, alikuwa amevalia sketi na blauzi nyekundu, zenye ‘material’ ya bazee na jamaa naye akiwa ametupia jinzi la bluu na shati rangi ya damu ya mzee.
Wakiwa wanaendelea na stori za hapa na pale huku wakionekana kuwa wamekolea kwa kinywaji, dada mmoja alipita eneo lile na kusimama kwa muda mrefu akiwakazia macho, jambo lililomfanya paparazi wetu kuachana na mambo mengine na kusubiria kitakachotokea.
TIMBWILI
Haikuchukua hata dakika tano, yule dada alirudi akiwa na kampani yake, huku mwanamke mmoja ambaye alijitaja kuwa ni mke wa njemba yule akimvamia yule dada na kuanza kumpa kichapo.
“Nimekuvumilia sana wewe malaya, kwa nini unaniharibia maisha yangu? Mume wangu hatulii nyumbani, mi nahangaika na watoto, wewe unakula raha huku. Tena usivyo na haya umevaa na nguo mpya kabisa za Valentine, leo utanitambua,” dada huyo alisikika akisema kwa sauti huku akiendelea kumpa kichapo.
Jamaa (mume) alipoona soo limekuwa kubwa, alitimua mbio na kuacha timbwili likiendelea.
AZIMIA
Kipigo kilikuwa kikali na kwa bahati mbaya watu walichelewa kuamulia ugomvi huo hali iliyosababisha mrembo aliyekuwa akichezea kichapo kupoteza fahamu.
Wasamaria wema walipoona hali imekuwa mbaya kiasi kile, waliwaamulia, kisha wakatoa taarifa kwa uongozi wa ukumbi ambapo viongozi walifika haraka na kuwakamata mwanamke aliyekuwa akitoa kichapo na wapambe wake.
WAFUMANIAJI MIKONONI MWA POLISI
Wakati walioanzisha vurumai lile wakiwa chini ya ulinzi huku mrembo yule akipepewa, baunsa mmoja wa ukumbi huo alitoka nje na kuwaita polisi ambao baada ya muda mfupi waliingia ukumbini humo.
Polisi hawakutaka kupoteza muda, waliwakamata wanawake hao kisha wakawatia pingu na kwenda nao kituoni.
Njiani, dada yule aliyekuwa amezimia alikuwa akiendelea kukupewa ili aweze kupata hewa na kuzinduka, jambo ambalo halikuzaa matunda.
Habari zilipopatikana baadaye zilieleza kuwa, wanawake wale walitiwa ndani baada ya kuchukuliwa maelezo yao wakati mrembo aliyechezea kichapo akipelekwa katika Hospitali ya Mkoa wa Kitabibu, Temeke, Dar kwa matibabu.
Zoezi hilo lilifanyika baada ya taarifa za mrembo huyo kuingizwa kwenye fomu ya polisi nambari tatu ‘(PF3), huku waliompa kichapo wakisubiri mrembo huyo apone ndipo shauri lao liendelee.
Hata hivyo, mrembo huyo alirejewa na fahamu muda mfupi baada ya kufikishwa hospitalini ambapo matibabu yalianza mara moja.

KASI YA MSANIIIII MARUFU,,,,,,,,,, LULU MICHAEL YAIBUKA TENAAAAAAAAAAAAA SOMA HAPA CHIN,,,,

 Lulu (katikati) akitoka eneo la mahakama baada ya kukamilisha dhamana yake.
Lulu akiwa ndani ya gari baada ya kukamilisha dhamana yake.
Kutoka kushoto ni mama mzazi wa Lulu Lucresia Karugila, wakili wa Lulu bwana Kibatala na Dk. Cheni wakijadili jambo wakati wakisubiri dhamana ya Lulu.
Lulu akiingia katika chumba cha msajili wa mahakama ili kukamilisha dhamana yake.
Gari lililombeba Lulu likiondoka mahakamani.
Lulu akishuka katika gari la polisi baada ya kuwasili mahakamani leo.
Lulu akiongea na wanahabari (hawapo pichani) baada ya kupata dhamana leo.
 --------------------------------
MAHAKAMA Kuu Kanda ya Dar es Salaam leo imemwachia kwa dhamana msanii wa filamu, Elizabeth Michael 'Lulu' aliyekuwa anakabiliwa na kesi ya kumuua msanii mwenzake wa filamu Steven Kanumba Aprili 7, 2012 bila kukusudia baada ya kukamilisha taratibu zote za dhamana.

Mvua yaua mmoja, yaezua nyumba 62 huko

mvua


Nyumba 62 zilizopo katika Vijiji vya Wilaya ya Kilindi, zimeezuliwa na nyingine kubomoka kutokana na mvua kubwa iliyoambatana na upepo mkali kunyesha kwenye maeneo mbalimbali ya Mkoa wa Tanga.
Maafa hayo yamesababisha mtoto mmoja kufa kwa kuangukiwa na nyumba, huku zaidi ya wanavijiji 110 kukosa mahala pa kuishi.
Kwa mujibu wa habari zilizopatikana na kuthibitishwa na Mkuu wa Wilaya ya Kilindi, Selemani Liwowa ni kuwa nyumba hizo zimeezuliwa usiku wa kuamkia Ijumaa wiki iliyopita baada ya kunyesha mvua iliyoambatana na upepo.
Gazeti hili lilijulishwa kuwa mvua kubwa ilinyesha katika vijiji mbalimbali vya wilayani hapa na kusababisha madhara hayo.
Akithibitisha tukio hilo, Liwowa alivitaja vijiji vilivyokumbwa na maafa hayo kuwa ni Songe, ambako mtoto mmoja amekufa kwa kuangukiwa na ukuta.
Vijiji vingine ni Kwasetemba, ambako nyumba 16 zimeanguka na Gitu zilikobomoka na kuezuliwa ni nyumba 42.
Alisema ya maafa hayo, Kamati ya Ulinzi na Usalama ya Wilaya Kilindi iliweza kutembelea kwa lengo la kujionea athari, ambapo hatua inayofuata ni kutuma wataalamu kutathimini athari na mahitaji kwa waathirika.

Kutana na Delfina Cedeno, Msichna wa Miaka 19 anayetoka Machozi na Jasho la Damu akiwa na Huzuni..!! soma zaid kujua,,,,,

machozi
Miaka minne iliyopita msichana huyu mwenye umri wa miaka 19, Delfina Cedeno, alianza kupata tatizo hili la ajabu, lililokuwa likimfanya alie na kutoka jasho la damu. Kwa kuongeza zaidi, wakati mwengine damu zimekuwa zikitoka hata kwenye kucha na kitovu.

Hali hii ilipomuanza, alianza kwa kulia machozi mekundu, kutokwa na damu puani na kunyunyukwa nywele kichwani.
 
Hali ilipokuwa mbaya, alikuwa akienda hedhi kwa siku 15 mpaka ikafika kipindi alihitaji kuongezwa damu kutokana na hali hiyo iliyokuwa ngumu. Licha ya vipmo vingi alivyofanya, madaktari wa mji wake wa Veron, kwenye Jamhuri ya Dominica, walishindwa  kumsaidia.
Cedeno alisema: ‘Hali hii ilipoanza kwangu sikuwa najua nini cha kufikiri – nilishtushwa na kuogopa.
Anasema alijisikia vibaya kutokana na hali aliyokuwa nayo mpaka ikambidi aondoke nyumbani kwao alipokuwa akiishi na mama yake aitwaye Mariana, 36.
Aliacha shule huku marafiki zake wengi wakimtenga kutokana na hali hiyo wakihofu kupata maambukizo au usumbufu kutokana na hali yake.
‘Nilitengwa, ila Mungu mkubwa. Kwa sasa najisikia poa maana baada ya muda mrefu nimeanza kujisikia vizuri.’
Miezi michache baadae alifanikiwa kupata boyfriend, Recaris Avila, ambaye alimtembelea hospitali mara baada ya kusikia stori yake.





Sasa, miaka minne baada yote kuanza, madaktari wa wamefanikiwa kutatua tatizo lake.



Wednesday, 6 November 2013

CHADEMA yapata pigo kufuatia kifo cha Ghafla cha Naibu Meya wake...!!



CHAMA cha Demokrasia na Maendeleo (CHADEMA) kimepata pigo baada ya Naibu Meya wa Manispaa ya Moshi, mkoani Kilimanjaro, Vicent Remoy, kufariki ghafla jana.

Akithibitisha kutokea kwa kifo hicho, Meya wa Manispaa hiyo, Jafary Michael (CHADEMA), alisema Remoy ambaye pia alikuwa ni Diwani wa Kata ya Kiboriloni, zahanati ya Jafary iliyoko katikati ya mji wa Moshi.
  
Ni kweli amefariki, na mimi nimepokea taarifa hiyo dakika 30 zilizopita, na kwa mujibu wa taarifa za awali, ni kwamba alienda kutizama afya yake hapo zahanati baada ya kuhisi kifua kuwa kizito wakati akiwa shambani kwake Msalanga,” alisema Michael.