Rais wa Italia, Giorgio
Napolitano, amepokea barua ya kujiuzulu kwa waziri mkuu, Enrico Letta.
Letta aliiwasilisha rasmi barua hiyo siku moja baada ya chama chake
kupiga kura kujitoa kwenye muungano wa utawala.
Wandani wake katika chama chake cha
Democratic ndio waliomfuta kazi. Hatua hiyo iliunga mkono changamoto
dhidi ya Letta kutoka kwa kinara mpya ambaye ni kijana mwenye maono
Matteo Renzi.Kitakacho fanyika sasa kimo mikononi mwa rais wa Italia, Napolitano.
Hata hivyo kuna uwezekano mkubwa wa rais huyo kumchagua Bw. Renzi kuwa waziri mkuu kisha aunde serikali.
Hicho kitakuwa kilele cha safari ya uongozi wake. Bw.Renzi aliye na umri wa miaka thelathini na tisa, hajawahi kuchaguliwa bungeni, wala kuitumikia serikali. Ni wazi kwamba hana uzoefu lakini ni analeta matumaini ya kuleta mageuzi.
0 comments:
Post a Comment