Showing posts with label ajali. Show all posts
Showing posts with label ajali. Show all posts

Wednesday, 19 February 2014

BREAKING NEWzz::Lori la Mafuta Lapinduka katika Mlima Sekenke na kuwaka Moto na Kuuwa Watu Wanne Joni yaLeo.

lori1 Lori la mafuta limeanguka jioni hii katika eneo la milima ya sekenke mkoani Singida na kuua watu wanne hapohapo.Chanzo cha ajali hiyo ni breki kufeli kukamata wakati lori hilo lilipokuwa linashuka mlima huo.Shuhuda wa ajali hiyo bwana Julius Chacha alipoongea na mtandao wetu wa Dj sek blog amesema kwamba Lori hilo lilipoacha njia lilipinduka na kuingia bondeni na kushika moto.Akiendelea kuongea shuhuda huyo alisema walishindwa kutoa msaada wowote kwa kuwa moto uliposhika ulikuwa mkubwa na hawakuwa na vifaa vya kuokolea.Watu wanne wamekufa papo hapo kutokana na ajali hiyo.Polisi walikuwa bado hawajafika eneoo la tukio mpaka tunaondoka eneo la tukio.

Baadhi ya Wananchi waliofika katika ajali hiyo wakiangalia mabaki ya Lori hilo baada ya kupata ajali na kuwaka moto leojioni likiwa katika safari zake za kusafirisha Mafyta nje ya Dar-es-Salaam, kupeleka mkoa wa jirani..


Mabaki ya Lori hilo baada ya kuteketea kabisa na moto jioni hii, baada ya kupata ajali katika eneo la mlima sekenke.

Baadhi ya wasafiri wakitazama lori lililongua jioni hii

Bonde la mlima sekenke linavyoonekana na baadhi ya miti imeunguaa
Hii ni njia ya mlima sekenke

Sunday, 16 February 2014

AJALI AJALI,,,,,,,MAJONZI MAKUBWA: AJALI MBAYA IRINGA, YAUWA WATU SITA WA FAMILIA MOJA WAFARIKI KATIKA AJALI IRINGA WAKIELEKEA MBEYA. SHUHUDIA


: GARI LILILOPATA AJALI TOYOTA RAV 4 T 770 BMP ENEO LA TANANGOZI -IRINGA LILILOKUWA LIKIENDESHWA NA  BWANA EZEKIEL MWAITELEKE  (MAREHEMU)  MAJIRA YA SAA SITA NA NUSU MCHANA NA KUSABABISHA VIFO VYA WATU WATANO WA FAMILIA MOJA PAPO HAPO DESEMBA 4, 2012  

BAADHI YA AKINA MAMA WASAMARIA WEMA WA TANANGOZI  IRINGA WAKIJARIBU KUMPEPELEA MMOJA WA MAJERUHI WA AJALI ILIYOTOKEA DESEMBA 4,2012 HUKO TANANGOZI IRINGA LIKIHUSISHA TOYOTA RAV 4 T 770 BMP LILILOINGIA NYUMA YA TRAILER  T 566 BNQ AMBAPO WATU WATANO WA FAMILIA MOJA WALIOKUWA WAKITOKEA DAR KWENDA MBEYA WALIFARIKI PAPO HAPO
6:BAADHI YA WASAMARIA WEMA WAKITOA MOJA YA  MAITI  KUTOKA KATIKA GARI TOYOTA RAV 4 T 770 BMP HUKO TANANGOZI IRINGA DESEMBA 4,2012 WATU WATANO WA FAMILIA MOJA WALIOKUWEMO KATIKA GARI HILO WALIFARIKI PAPO HAPO(PICHA ZOTE NA MISANJO LIVIGHA (MLALAHOI ALWATAN WWW.FRANCISGODWIN.BLOGSPOT.COM

 GARI AINA YA SCANIA LENYE CABIN NA. T 840 BST LIKIWA NA TRAILER NAMBA  T 566 BNQ LILIGONGWA KWA NYUMA NA TOYOTA RAV 4 T 770 BMP HUKO TANANGOZI IRINGA NA KUSABABISHA VIFO VYA WATU WA TANO WA FAMILIA MOJA PAPO HAPO  WALIOKUWA KATIKA GARI HILO RAV 4
Ajali  mbaya  imetokea  mkoani Iringa mchana  wa  leo na kusababisha  vifo  vya  watu  wanne  wa familia  moja  pamoja na mfanyakazi  wa ndani mmoja.

Ajali  hiyo  imetokea katika  eneo la Tanangozi  wilaya ya  Iringa kwenye kizuizi cha barabara  cha mafundi wa kutengeneza barabara  kuu ya Iringa -Mafinga  mkoani Iringa mida ya saa nane mchana

Kwa mujibu  wa mashuda  wa  tukio   hilo  wameueleza  mtandao  huu  wa  www.francisgodwin.blogspot.com  kuwa  chanzo  cha ajali  hiyo ni dereva wa gari dogo aina ya Rav 4  lenye namba  za usajili T 770 BMP kulipalamia lori  lenye tela kwa nyuma. 
Huku  chanzo kikitajwa  kuwa ni kuendesha  kwa mwendo kasi  wa  dereva  wa gari ndogo marehemu Ezekiel Mwaiteleke  na kushindwa  kulimudu na kulipalamia lori kwa nyuma.
Kwa mujibu  wa mashuda  wa  tukio   hilo  wameueleza    kuwa  chanzo  cha ajali  hiyo ni dereva wa gari dogo aina ya Rav 4 kuendesha  kwa mwendo kasi na kushindwa  kulimudu na kulipalamia lori kwa nyuma na kuwa  gari hiyo ilikuwa ikitokea  jijini Dar es Salaam kwenda Kyela mkoani Mbeya.

Hivyo katika ajali  hiyo  abiria  wote  wanne akiwemo baba na mama  wa  watoto  wawili  waliokuwemo katika gari  hiyo pamoja na  watoto hao  kufa papo hapo na maiti  zote  kupelekwa katika Hospitali ya mkoa wa Iringa.

 Majina ya  waliokufa  ni pamoja  na Ezekiel Mwaiteleke ambaye ni dereva  wa gari hilo na baba  wa familia  hiyo ,mkewe Grace Mwaiteleke ,mtoto Kelvin Mwaiteleke (2),Happy Mwandike na mfanyakazi  wao  wa ndani aliyefahamika kwa jina la Linda Ezekiel  huku majeruhi katika ajali  hiyo ni mmoja na amekimbizwa  Hospital ya mkoa  wa Iringa.

Saturday, 15 February 2014

Alichokiandika msanii KALA JEREMIAH baada ya kunusurika Kifo hapo Jana..!!



kala
Leo Kala Jeremiah kupitia ukurasa wake wa Instagram amepost picha inayoonyesha ajali aliyoipata wakati akitokea kwenye show yake iliyokuwa ikifanyika Club East 24 ambayo alikua akifanya show pamoja The B Band ya Banana Zoro.
IMEPATA AJALI USIKU HUU NIKIWA NATOKEA CLUB EAST 24 AMBAKO NILIKUWA NAFANYA SHOW NA B BAND WAKATI NARUDI NYUMBANI GHAFLA KUNA MTU WA PIKIPIKI AKAWA ANATAKA KUINGIA NIKAJARIBU KUMKWEPA GARI ILIKUA MWENDO KASI KIDOGO IKAYUMBA KWENDA KULIA NIKAIRUDISHA IKARUDI ZAIDI KUSHOTO NIKAIRUDISHA TENA KULIA IKAWA INATAKA KWENDA MTARONI NIKAIRUDISHA TENA KUSHOTO AMBAKO ILIGEUKA ILIKUKUA INATOKA NA KUINGIA MTARONI AMBAKO ILIKITA NA KUVUNJA MLANGO WA UPANDE WANGU.SIJAAMINI KAMA NIMETOKA BILA HATA JERAHA MGUUNI WALA MAUMIVU ZAIDI YA YALE UA KICHWANI KIDOGO NILIYOJIGONGEA KWENYE MLANGO KWA JUU.AHSANTE SANA MUNGU UMENIOKOA.ASANTE SANA MUNGU WANGU.

Wednesday, 6 November 2013

PICHA ZINATISHA ...AJALI MBAYA YA PIKIPIKI YAUA HUKO MWANZA


Watu wawili wamefariki dunia papo hapo wilayani Bukombe mkoani Geita wakitumia usafiri wa bodaboda kufuatia pikipiki waliyokuwa wakisafiria kuteleza kwenye mchanga ikiwa kwenye mwendo kasi na kisha kukanyagwa vibaya vichwani na gari aina ya Noah ambayo walikuwa wakipishana nayo.