Umati wa watu waliofika katika eneo la kitanzini kuangalia handaki hilo
mkuu wa Wilaya Ya Iringa mjioni Dkt Leticia Warioba akihojiana na mmiliki wa numba ambayo handaki hilo limeonekana
Handaki lenyewe muonekano wa sehemu ya kuingilia
Mkuu wa Wilaya kushoto aipokea maelekezo kutoka kwa mmoja wa wafanyakazio wa kampuni ya maji Iringa
Wananchi wakendelea kutazama kila mmoja akiwaza lake
Handaki la ajabu limeonekana katika eneo la kata ya kitanzini mtaa wa sokoni
Katika tukio hilo lililokuwa gumzo kubwa katika eneo hilo huku kila mmoja akisema lake
Mtandao
huu ulipokutana na mmiliki wa nyumba hiyo hakuweza kuwa na majibu
yakuridhisha huku akisema yeye hafahamu shimo hilo limetokea wapi.
Handaki
hilo ambalo lilionekana jana na wachimbaji wa mitaro wa JR
wanaoshuhulika na uwekwaji wa mabomba mapya ya maji safi wanaeleza
katika kuchimba ndipo walipokutana na chemba hiyo ikiwa imefunikwa na
kudhani kuwa inatumika kama shimo la choo ya nje lakini haikuwa hivyo
maana lilikuwa wazi limejengewa na hakuna dalili ya kutumika kama choo.
Akizungumza
mmoja wa wananchi aliyeingia katika handaki hilo Abdukareem ameeleza
kuwa yeye ni mkazi wa eneo hilo na alipopata taarifa alifika akiwa na
mwenzake aliyefahamika kwa jina la Salehe na kukubaliana kuingia ndani
ili kufahamu kilichopo.
Ameeleza
kutokana na shimo hilo kuwa refu walitafuta ngazi lakini hawakufanikiwa
kwani ngazi hiyo ilikuwa pana na kuamua kutafuta fimbo kubwa ya muanzi
na kamba na ndipo walipofanikiwa kuingia ndani.
Anazidi
kueleza kuwa walipofika ndani walikuta chumba ambacho ni kama futi tatu
na kuona vidirisha vidogo kwa mbele huku bado kukiwa kumejengewa kwa
zege na kubainisha kuna muendelezo wa chemba nyingine ambapo hawakuweza
kuendelea kutokana na kuzibwa.
mkuu wa Wilaya afika eneo la tukio
Mkuu
wa wilaya ya Iringa Dkt Leticia Warioba akafika katika eneo la tukio
huku akiwa na wa wafanyakazi wa Kampuni ya JR pamoja na afisa wa
usalama ambao waliishia kuangalia njia hiyo pasipo kuingia ndani ya
handaki hilo.
nini maoni ya wakazi waliofika katika eneo hilo?
Wengi
wa wakazi waliofika katika eneo hilo hawakusita kueleza hisia zao huku
wengine wakieleza labda ni mahandaki yaliyokuwa yakitumiwa na Wajerumani
enzi za ukoloni, huku wengine wakieleza labda handaki hilo limekuwa
likitumiwa na majambazi kama sehemu za kujificha na kuhifadhia mali
walizoiba japo hapakuonekana na mali aina yeyote.
0 comments:
Post a Comment