Mwanamke mmoja ambaye alifahamika kwa jina la Rashushi Amani Shembusho, mkazi wa Pasua, wilaya ya Moshi, mkoani Kilimanjaro, ametapeliwa kiasi cha shilingi milioni 5.4 na watu wasiojulikana asubuhi ya jana, Februari 20.
Bi. Shembusho akilia kwa uchungu baada ya
kudangasnywa na watu wawili, wa kike na wakiume ambao majina yao bado
hayajafahamika. watu hao walimpeleka katika Hoteli maarufu mjini moshi,
Fresh Coach na kumtapeli shilingi milioni 5.4 ambazo alikuwa ametoka kutoa Benki ya Uchumi ya mjini Moshi.
Askari
wa Hoteli hiyo inayodaiwa kutumika kumtapeli mwanamke huyo akimtuliza
Mama huyo ambaye alionekana kuchanganyikiwa na tukio hilo.Mama akilia kwa uchungu.. Keleuwieeeeeee...!!!!!Msamaria
Mwema aliyefika katika eneo la tukio na kujitolea kumpeleka Mwanamke
huyo katika kituo cha Polisi cha Kati cha Mjini Moshi.Mama akisimulia tukio zima kwa wananchi waliofika katika eneo la tukio baada ya kumsikia akipinga ukunga kuomba msaada.Msamaria
Mwema aliyefika katika eneo la tukio na kujitolea kumpeleka Mwanamke
huyo katika kituo cha Polisi cha Kati cha Mjini Moshi.Bi. Shembusho akipanda gari la Msamaria Mwema aliyejitolea kumpeleka Polisi kutoa taarifa hizo. Na Dixon Busagaga wa globu ya jamii Moshi.
0 comments:
Post a Comment