Akizungumza na waandishi wa habari jana katika ofisi za kituo hicho zilizopo Mwenge jijini Dar es Salaam, Mkurugenzi Mtendaji wa TCIB, Deus Kibamba, alisema kauli ya Rais Kikwete kuwataka wafuasi wa Chama Cha Mapinduzi (CCM) waamke na kujibu mapigo wanaposhambuliwa, ni uchochezi.
Alisema tayari ametoa taarifa kwa Mwendesha Mashitaka Mkuu wa ICC, Fatou Bensuda, kumwomba atume timu yake nchini ili ifanye uchunguzi wa awali juu ya matamshi ya viongozi wakuu nchini.
0 comments:
Post a Comment