MAHABUSU,
Vumi Elias (30), amefariki dunia baada ya kujinyonga kwa kutumia
tambala la kupigia deki ndani ya choo cha mahabusu ya Kituo cha Polisi
Tunduma.
Elias, mkazi wa Maporomoko-Tunduma, aliyetuhumiwa kwa unyang’anyi wa
kutumia nguvu katika eneo la Tunduma wilayani Momba, alifariki dunia
jana, saa 12 asubuhi muda mfupi baada ya kufikishwa katika Kituo cha
Afya Tunduma kwa matibabu.
Kaimu Kamanda wa Polisi mkoani Mbeya, Robert Mayala, alisema Elias
aliingia choo cha mahabusu saa 10 alfajiri na kufanya jaribio la
kujinyonga kwa kutumia nguo ya kupigia deki.
0 comments:
Post a Comment