Monday, 17 February 2014

LULU Alikumbuka Penzi La KANUMBA Siku ya VALENTINE DAY….Afunguka ya Moyoni.

lulu
WAKATI kesi yake juu ya kifo cha aliyekuwa nyota wa filamu Bongo, Steven Kanumba ikianza kurindima leo katika Mahakama Kuu Kanda ya Dar es Salaam, mwigizaji Elizabeth Michael ‘Lulu’ ametoa la moyoni akikumbuka mapenzi ya jamaa huyo aliyetangulia mbele za haki.
Lulu alifunguka hayo mwishoni mwa wiki iliyopita, Siku ya Wapendanao (Valentine’s Day) iliyosherehekewa duniani kote Ijumaa iliyopita.
“Kuna mtu natamani kumtakia Happy Valentine’s Day kwa kuwa nakumbuka mapenzi yake kwangu lakini kwa bahati mbaya siwezi kwa sababu hayupo na haiwezekani tena,” alisema Lulu.

Elizabeth Michael ‘Lulu’.


Marehemu Steven Kanumba.

0 comments:

Post a Comment