GARI
AINA YA SCANIA LENYE CABIN NA. T 840 BST LIKIWA NA TRAILER NAMBA T
566 BNQ LILIGONGWA KWA NYUMA NA TOYOTA RAV 4 T 770 BMP HUKO TANANGOZI
IRINGA NA KUSABABISHA VIFO VYA WATU WA TANO WA FAMILIA MOJA PAPO HAPO
WALIOKUWA KATIKA GARI HILO RAV 4
Ajali
mbaya imetokea mkoani Iringa mchana wa leo na kusababisha vifo
vya watu wanne wa familia moja pamoja na mfanyakazi wa ndani
mmoja.
Ajali
hiyo imetokea katika eneo la Tanangozi wilaya ya Iringa kwenye
kizuizi cha barabara cha mafundi wa kutengeneza barabara kuu ya Iringa
-Mafinga mkoani Iringa mida ya saa nane mchana
Kwa
mujibu wa mashuda wa tukio hilo wameueleza mtandao huu wa
www.francisgodwin.blogspot.com kuwa chanzo cha ajali hiyo ni dereva
wa gari dogo aina ya Rav 4 lenye namba za usajili T 770 BMP
kulipalamia lori lenye tela kwa nyuma.
Huku
chanzo kikitajwa kuwa ni kuendesha kwa mwendo kasi wa dereva wa
gari ndogo marehemu Ezekiel Mwaiteleke na kushindwa kulimudu na
kulipalamia lori kwa nyuma.
Kwa
mujibu wa mashuda wa tukio hilo wameueleza kuwa chanzo cha
ajali hiyo ni dereva wa gari dogo aina ya Rav 4 kuendesha kwa mwendo
kasi na kushindwa kulimudu na kulipalamia lori kwa nyuma na kuwa gari
hiyo ilikuwa ikitokea jijini Dar es Salaam kwenda Kyela mkoani Mbeya.
Hivyo
katika ajali hiyo abiria wote wanne akiwemo baba na mama wa
watoto wawili waliokuwemo katika gari hiyo pamoja na watoto hao
kufa papo hapo na maiti zote kupelekwa katika Hospitali ya mkoa wa
Iringa.
Majina
ya waliokufa ni pamoja na Ezekiel Mwaiteleke ambaye ni dereva wa
gari hilo na baba wa familia hiyo ,mkewe Grace Mwaiteleke ,mtoto
Kelvin Mwaiteleke (2),Happy Mwandike na mfanyakazi wao wa ndani
aliyefahamika kwa jina la Linda Ezekiel huku majeruhi katika ajali
hiyo ni mmoja na amekimbizwa Hospital ya mkoa wa Iringa.
0 comments:
Post a Comment