Katibu Mkuu Wizara ya
Habari, Vijana, Utamaduni na Michezo, Bi. Sihaba Nkinga, akisisitiza jambo, leo
Novemba 5, 2013, jijini Dar-es-salaam, alipokutana na ujumbe wa kampuni ya
Symbion ya Marekani kujadili maandalizi ya ujenzi wa kituo kikubwa cha
maendeleo ya mchezo wa soka nchini (Soccer Academy), ambayo itashirikiana na
Club ya Sunderland ya Uingereza katika kuindesha Academy hiyo. Katika
mpango huo, Kampuni ya Symbion pia itajenga viwanja vya michezo (sports
courts) eneo la Kidongo Chekundu. Mazungumzo hayo yamehusisha pia ujumbe wa
viongozi kutoka Idara ya Michezo (hawapo pichani)