Showing posts with label makala. Show all posts
Showing posts with label makala. Show all posts

Monday, 17 February 2014

Kigogo wa CCM Ataja Siri Mpya ya Wauzaji Dawa za Kulevya.

sembe
MBUNGE wa Kigamboni, Faustine Ndungulile ameanika siri na aina mpya ya wauzaji wa dawa za kulevya wanayoitumia katika kupanua wigo wa watumiaji wa madawa ya kulevya Duniani kupitia watoto wadogo. Ndungulile aliyasema hayo wakati akifungua Baraza la Vijana la Umoja wa vijana wa Chama Cha Mapinduzi (UVCCM) kupitia wilaya ya Temeke uliofanyika katika ukumbi wa Malaika, ambapo alibainisha bayana wauzaji wa madawa ya kulevya wamekuja na mtindo mpya wa kuwafundisha watoto wadogo kutumia madawa ya kulevya kupitia kwenye vyakula wanavyopewa wakiwa shuleni pamoja na kwenye pipi ambazo watoto hao wanapozilamba taratibu huanza kujifunza kutumia dawa za kulevya na hata siku za usoni inawawia vigumu kuacha matumizi ya dawa hizo.
“Wauzaji wa madawa ya kulevya ni watu hatari sana kwani siku hizi wameanzisha mtindo wa kuwachanganyia watoto wadogo kwenye vyakula pamoja na kuyapaka madawa hayo ya kulevya kwenye pipi ambazo watoto hao wanapozilamba huanza kujifunza matumizi ya madawa ya kulevya tangu wakiwa watoto na ni ngumu kuchomoka katika mtego wa matumizi ya madawa hayo katika maisha yao”, alisema Ndugulile.
Kama haitoshi Ndungulile alianika bayana matatizo makubwa yanayowasibu vijana kwa sasa kuwa ni madawa ya kulevya pamoja na maambukizi ya virusi vya ukimwi ambapo alibainisha waziwazi kuwa nguvu kazi ya taifa la leo imekuwa rehani kupitia mitego hiyo. Mbunge huyo wa Kigamboni ambaye kitaaluma ni Daktari aliweka waziwazi kuwa licha ya takwimu za kushuka kwa maambukizi ya virusi vya ukimwi kushuka kutoka asilimia 7 mpaka asilimia 5.1 bado tatizo ni kubwa kupita maelezo kwa vijana nchini.
sembe
“Kati ya vijana wa kike watatu wanaotumia madawa ya kulevya, wawili kati yao ambao ni asilimia 67 wameathirika na virusi vya ukimwi. Halikadhalika kwa upande wa vijana wa kiume wawili wanaotumia madawa ya kulevya, mmojawao ambaye ni asilimia 50 ana maambukizi ya virusi vya ukimwi. Hali ni mbaya sana kwa vijana.” Alisema Ndungulile.
Mbunge huyo wa Kigamboni aliwaasa wajumbe hao wa Baraza la UVCCM (W) Temeke na vijana wote nchini kuwa mbali na matumizi ya madawa ya kulevya na badala yake wajibiidishe zaidi katika kufanya mambo yenye faida kwao kupitia shughuli za kiuchumi kwa kuchangamkia fursa zilizopo.
 Mjumbe wa Baraza la UVCCM, Ndugu Emmanuel John akichukua karatasi ya kupigia kura.
Wakati huo huo, Umoja wa Vijana wa Chama Cha Mapinduzi (UVCCM) wilaya Temeke wamefanya uchaguzi wa majimbo yaliyopo ndani ya Wilaya hiyo na kupata Wenyeviti na Makatibu wapya wa majimbo. Baraza hilo la Vijana ambalo lilifunguliwa na Mgeni rasmi Mbunge wa Kigamboni, Faustine Ndungulile ambaye wakati wa ufunguzi aliwaasa vijana kujiepusha na matumizi ya madawa ya kulevya na kujikinga zaidi na maambukizi ya virusi vya ukimwi kwani hali iliyopo inatisha sana kwa vijana.
“Kati ya vijana wa kike watatu wanaotumia madawa ya kulevya, wawili kati yao ambao ni asilimia 67 wameathirika na virusi vya ukimwi. Halikadhalika kwa upande wa vijana wa kiume wawili wanaotumia madawa ya kulevya, mmojawao ambaye ni asilimia 50 ana maambukizi ya virusi vya ukimwi. Hali ni mbaya sana kwa vijana.” Alisema Ndungulile.
Ndugu Ndungulile ambaye pia ni Mjumbe wa kamati ya siasa ya wilaya ya Temeke aliwaasa na kuwatia moyo vijana kujitokeza kugombea nafasi mbalimbali za kiuongozi katika uchaguzi wa serikali za mitaa  na uchaguzi mkuu hapo mwakani naye kwa nguvu zake zote atapambana katika kuwatetea vijana wenye sifa stahiki kwani anaamini vijana ni nguvu kazi ya sasa ya Taifa.
Ndugu Ndugulile aliwaasa na kuwatakia uchaguzi mwema wajumbe wa Baraza hao wachague viongozi wenye sifa wanaowataka kwani yeye kama Ndugulile ameanika wazi kuwa hajashiriki kupanga safu za viongozi badala yake jukumu hilo limeangukia mikononi mwa wajumbe.
Kwenye baraza hilo la Vijana ambalo lilikuwa ni baraza la kazi wamechagua viongozi wa majimbo ya Kigamboni na Temeke yanayopatikana ndani ya Wilaya ya Temeke. Kwa upande wa Temeke waliojitokeza kuomba nafasi ya Uenyekiti ni Arnord Sangawe aliyepata kura 48, Julius Mkada aliyepata kura 24 na Peter Sillo aliyepata kura 4. Mshindi wa nafasi ya Uenyekiti wa Jimbo la Temeke UVCCM ulinyakuliwa na Arnord Sangawe. Waliojitokeza kwenye nafasi ya Ukatibu walikuwa ni Athumani Nyamlani aliyepata kura 6, Juma Ndwangila aliyepata kura 59 pamoja na Laurence Limwata aliyeapata kura 11. Hivyo nafasi ya Ukatibu kuchukuliwa na Juma Ndwangila.
Kwa upande wa jimbo la Kigamboni wagombea wa nafasi ya Uenyekiti wa jimbo walikuwa ni Ally Makwilo aliyepata kura 28, Shaaban Mbegu aliyepata kura 7 na Yasin Kanyama aliyepata kura 43. Hivyo Yasin Kanyama akatangazwa ndiye mshindi wa Uenyekiti wa Jimbo la Kigamboni kupitia UVCCM.
Halikadhalika upande wa makatibu wagombea wa jimbo la Kigamboni walikuwa ni Kambarage Makongoro aliyepata kura 27, Mustaffa Pilla aliyepata kura 32 na Salum mpili aliyepata kura 16 na matokeo hayo yalimpa ushindi Ndugu Mustafa Pilla kuwa ndiye Katibu wa jimbo la Kigamboni kupitia UVCCM.

MAAJABU HAYA ..!! KAMA BADO BASI MTAZAME MREMBO MWENYE KIUNO CHEMBAMBA KULIKO WAREMBO WOTE DUNIANI...


Cathie Jung ana miaka 77 na ndiye mwanamke mwenye kiuno chembamba zaidi Duniani. 
 Yumo miongoni mwa watu kwenye kitabu maarufu cha kumbukumbu za Guinness worldHakika hii inashangaza kimtindo.

Cheki picha zaidi hapo chini...



Sunday, 16 February 2014

Arusha: Polisi wakamata magunia mengine 97 ya bangi



Kamanda wa Polisi Mkoa wa Arusha Kamishna Msaidizi wa Polisi, Liberatus Sabas akiwaonyesha waandishi wa habari madawa ya kulevya aina ya bangi ambayo yalikuwa kwenye magunia 97 yaliyokamatwa na askari wa jeshi hilo katika eneo la Usa River wilayani Arumeru.
Taarifa na Na Rashid Nchimbi wa Jeshi la Polisi Arusha

Jeshi la Polisi mkoani hapa limemkamata mtu mmoja akiwa na magunia 97 ya madawa ya kulevya aina ya bangi ambayo yalikuwa yanasafirishwa toka mkoani hapa kuelekea Moshi. Akithibitisha kutokea kwa tukio hilo, Kamanda wa Polisi Mkoa wa Arusha Kamishna Msaidizi wa Polisi Liberatus Sabas amesema kwamba, tukio hilo lilitokea muda wa saa 10:00 alfajiri eneo la Usa River wilayani Arumeru.

Alisema mafanikio hayo yametokana na ushirikiano mzuri kati ya jeshi hilo na wananchi ambapo taarifa za tukio hilo zilitolewa na raia wema ambapo askari wa jeshi hilo waliweka mtego eneo hilo na kufanikiwa kulikamata gari aina ya Fuso lenye namba za usajili T. 282 AAJ.

Kamanda Sabas aliongeza kwa kusema kwamba, ndani ya bodi ya gari hilo kulikuwa na mboga aina ya kabeji iliyosambazwa vizuri huku chini ya mboga hiyo kukiwa na madawa hayo yaliyokuwa kwenye magunia huku yakivingirishwa kwenye mifuko ya “plastiki” kwa ndani.

Alisema katika gari hilo kulikuwa na watu watatu na mara baada ya askari hao kulisimamisha dereva pamoja na msaidizi wake walifanikiwa kukimbia huku mtu mmoja aliyejulikana kwa jina la Praygod Marick (22) Mkazi wa Dar esalaam akikamatwa.

Jeshi la polisi Mkoani hapa linaendelea kumhoji mtuhumiwa huyo huku watuhumiwa wengine wakiendelea kutafutwa. Kwa mara nyingine tena Kamanda huyo aliendelea kuwashukuru wananchi wa Mkoa huu kutokana na ushirikiano wao mkubwa wanaoutoa kwa jeshi hilo na kuendelea kuwasisitizia kuimarisha mahusiano na jeshi hilo.

Kwa muda wa kipindi cha mwezi mmoja toka januari 07, 2013 mpaka hivi leo jeshi hilo limeshakamata madawa ya kulevya aina ya mirungi magunia 372 katika magari mawili tofauti na pia limeshakamata jumla ya magunia 117 ya madawa ya kulevya aina ya bangi ambapo mwanzoni mwa wiki hii jumla ya magunia 20 yalikamatwa yakiwa yanasafirishwa kwa kutumia wanyama aina ya Punda maeneo ya Losoiti wilayani Longido.

Saturday, 15 February 2014

Lowassa, Sumaye, Ngeleja wajieleza Kamati ya Mangula


Mawaziri wakuu wa zamani, Frederick Sumaye (kulia) na Edward Lowassa wakizungumza Mjini Dodoma jana kabla ya kuhojiwa na Kamati Ndogo ya Maadili ya CCM.



Dodoma.Waliowahi kuwa Mawaziri Wakuu; Edward Lowassa na Frederick Sumaye jana walifika mbele ya Kamati Ndogo ya Maadili ya CCM kutoa maelezo juu ya tuhuma za kufanya kampeni za urais kabla ya wakati.
Mbali na wastaafu hao, mwingine ambaye jana alifika mbele ya kamati hiyo ambayo ilikuwa chini ya Makamu Mwenyekiti wa CCM Bara, Philip Mangula na Katibu Mkuu wa chama hicho, Abdulrahman Kinana ni Waziri wa Nishati wa zamani na Mbunge wa Sengerema, William Ngeleja.
Mjumbe mwingine wa kamati hiyo aliyehudhuria kikao hicho kilichofanyika kwenye Ukumbi wa White House jana ni Waziri wa Nchi, Ofisi ya Waziri Mkuu (Sera, Uratibu na Bunge), William Lukuvi. Wajumbe wengine ni Dk Maua Daftari, Shamsi Vuai Nahodha na Pindi Chana ambao hata hivyo, hawakuhudhuria.
Hata hivyo, wanachama wengine watatu, Waziri wa Mambo ya Nje na Ushirikiano wa Kimataifa, Benard Membe, Waziri wa Nchi (Ofisi ya Rais Uhusiano na Uratibu), Stephen Wassira na Naibu wa Sayansi na Teknolojia, January Makamba ambao wote wanatazamiwa kuitwa leo mbele ya kamati hiyo.
Vyanzo kutoka ndani ya chama hicho vilieleza kuwa Membe alikuwa katika ziara ya Rais Jakaya Kikwete na alitarajiwa kurejea nchini jana jioni.
Akizungumza na waandishi wa habari mara baada ya kukamilika kwa mahojiano ya makada hao watatu jana, Kinana alisema shughuli ya kuwahoji wengine itaendelea leo.
“Kazi haijakwisha, kesho (leo) tunaendelea.”
Waliyosema baada ya kuhojiwa
Akiwa amevalia mavazi rasmi ya CCM, Lowassa alihojiwa kwa takriban saa moja na nusu kwani aliingia katika kikao hicho saa 4:56 asubuhi na kutoka saa 6:40 mchana akiwa ametumia takriban saa moja na nusu na alitoka akiwa mwenye furaha.
Alipoulizwa kuhusu mahojiano hayo Lowassa: “Mazungumzo yalikwenda vizuri. Yalikuwa na lengo la kujenga chama kwa ajili ya Uchaguzi Mkuu wa mwaka 2015,” alisema Lowassa huku akitabasamu.
Muda mfupi baada ya Lowassa kutoka, Sumaye aliingia kuanzia saa 6:46 na kutoka saa 8:05.
Baada ya kutoka, Sumaye pia hakuwa tayari kuzungumzia kuhusu mahojiano hayo... “Tunawasubiri wakubwa watakavyotoa jawabu.” Alipoulizwa sababu za kutumia muda mwingi katika kikao hicho alisema: “Tulikuwa tunakunywa chai.”

Nape atofautiana na Jaji Warioba Bunge la Katiba


Katibu wa Itikadi na Uenezi wa Chama Cha Mapinduzi (CCM), Nape Nnauye.PICHA|MAKTABA 
Na Fidelis Butahe, Mwananchi
Kwa ufupi
Akizungumza na gazeti hili jana, Nape alisema: “Mchakato wote wa Katiba Mpya unasimamiwa na sheria na sio maneno ya Warioba. Sheria inazungumzia haki, wajibu na mamlaka ya Bunge hilo, hivyo inawezekana kabisa kuboreshwa na hata kubadilishwa kwa hoja.”Share


Dar es Salaam. Katibu wa Itikadi na Uenezi wa Chama Cha Mapinduzi (CCM), Nape Nnauye, amesema Bunge Maalumu la Katiba, litatekeleza majukumu yake kwa kufuata Sheria ya Mabadiliko ya Katiba na si mawazo ya mtu yeyote.
Kauli hiyo ya Nape imekuja siku moja baada ya Mwenyekiti wa Tume ya Mabadiliko ya Katiba, Jaji Joseph Warioba kusema kuwa litakuwa jambo lisilo la kawaida kwa Bunge hilo kubadili hoja ya msingi iliyopo kwenye Rasimu ya Katiba, akisisitiza kuwa jukumu lake ni kuifanyia marekebisho.
Warioba alisema hayo juzi alipokuwa akizungumza katika mkutano ulioandaliwa na Kituo cha Demokrasia Tanzania (TCD), kuhusu tafakuri na maridhiano kuelekea katika Katiba Mpya.
Alisema kama Bunge Maalumu la Katiba likipewa jukumu la kuandika Katiba linaweza kubadili mambo mengi, lakini kama Katiba itakuwa imeandaliwa na chombo kingine, Bunge hilo linatakiwa kutobadili hoja za msingi.
Akizungumza na gazeti hili jana, Nape alisema: “Mchakato wote wa Katiba Mpya unasimamiwa na sheria na sio maneno ya Warioba. Sheria inazungumzia haki, wajibu na mamlaka ya Bunge hilo, hivyo inawezekana kabisa kuboreshwa na hata kubadilishwa kwa hoja.”
Nape alisema kulingana na sheria hiyo, Bunge hilo lina mamlaka ya kufanya jambo lolote katika Rasimu hiyo, ikiwa ni pamoja na kuifanyia maboresho kadri itakavyoonekana kuwa inafaa.
“Bunge haliwezi kutishwa na mtu yeyote kwa sababu lipo kwa ajili ya kuwawakilisha wananchi. Ndiyo maana baada ya Bunge hilo kwisha wananchi watapiga kura ya maoni,” alisema.
Akitolea ufafanuzi kauli ya Jaji Warioba kwamba Bunge hilo lifanye maboresho na si kubadili hoja za msingi, Nape alisema: “Maboresho maana yake ni kubadili. Ukiwa na nyumba ya vyumba vinne na kuiboresha kwa kuweka chumba kimoja si umeibadili?”
Alisema Bunge hilo linatakiwa lisiingiliwe katika uamuzi wake.

Maajabu ya ‘Shimo la Mungu’ Newala

 
Mkazi wa Newala, Maimuna Pinda  akionyesha eneo la ‘Shimo la Mungu’, sehemu ambayo pia wenyeji wa wilaya hiyo hufanyia matambiko.
Kwa ufupi
  • Asili yake ni kitendawili, yadaiwa ndege haziwezi kuruka juu yake

Newala. Katika Wilaya ya Newala, mkoani Mtwara lipo shimo la ajabu lijulikanalo kama ‘Shimo la Mungu’ lililochukua robo tatu ya ukubwa wa wilaya hiyo.
Shimo hili linalotajwa kuwa moja ya vivutio mkoani Mtwara limesheheni hifadhi za misitu, mito, mabonde, mawe ambayo yanapendeza kwa macho pia kipo kisima cha maji Newala.
Jambo hili linawasumbua wale wanaojua historia yake ni taarifa za kutupwa kwa watoto, kupotea kwa watu wale wanaojaribu kuingia bila ruhusu, wabishi wasioamini tambiko na mambo mengine kadhaa ambayo hata hivyo ni vigumu kuyathibitisha.
Ni shimo la asili ambalo limekuwapo miaka mingi, na wenyeji wa Mji wa Newala wanaliita ‘Shimo la Mungu’ kutokana na kile wanachoeleza kuwa ni maajabu ambayo hutokea yakianzia katika shimo hilo.
Miongoni mwa maajabu hayo ni yale ambayo hutokea nyakati za asubuhi kipindi cha masika ambapo upepo mkali sana huvuma kutoka lilipo shimo hilo.
Wanasema wakati mwingine hutokea moshi mzito ambao husambaa na kuufunika Mji wa Newala na kusababisha giza nene katika makazi ya watu kiasi cha watu kushindwa kuonana kwa kati ya dakika tatu na dakika saba.
Mkazi wa Newala, Sophia Saidi (90) anasema: “Sisi tumezaliwa tumelikuta, kutokana na shimo hilo kutotengenezwa na mtu yeyote ndio maana tukaliita ‘Shimo la Mungu”.
Bibi Sophia kama anavyojulikana na wengine anasema anaongeza: “Sehemu hiyo huwa panatokea miujiza kama hiyo ambayo inaleta upepo mkali, mara giza hata sisi hatujuwi ni nani ambaye ana sababisha kuwe na giza kutoka sehemu ya shimo hilo hadi sehemu ya makazi ya watu”.
Kutokana na umaarufu wake, eneo hilo limekuwa kivutio kikubwa cha watu ambao hufika kwa ajili ya kufanya matambiko ya jadi, ikiwa ni sehemu ya mila na desturi za wakazi wa Newala na wilaya nyingine jirani.
Maimuna Pinda (55) ambaye pia ni mwenyeji wa eneo hilo anasema hata waganga wa jadi kuingia na kutoka ndani ya ‘Shimo la Mungu’ kwa ajili ya kuchukua dawa mbalimbali za miti shamba ambazo hutumika kutibia magonjwa kadhaa. Pinda anasema kabla ya mtu hajaingia ndani ya shimo hilo ili kutalii au kuchukua dawa, lazima afanywe tambiko.
Pembezoni mwa shimo hilo huota uyoga ambao ni kitoweo kwa wakazi wanaolizunguka, lakini kwa maelezo ya wenyeji uchumaji huo huwa ni hatari kwani mara kadhaa watu wamepoteza maisha kutokana na kupatwa na kizunguzungu kisha kutumbukia kwenye shimo.

MWESHIMIWA RAIS kIKWETE: KABAINI KUNA MAJANGILI PAPA 40 NCHINI




Rais wa Tanzania Jakaya Kikwete akizungumza na mtangazaji wa kituo cha  televisheni cha  CNN, Christiane Amanpour jijini London. Picha na Ikulu 
Na Waandishi wetu, Mwananchi
  • Akihojiwa juzi jioni na Idhaa ya Kiswahili ya BBC, Rais Kikwete alikanusha taarifa zilizotolewa na gazeti la Sunday Mail la Uingereza zilizodai Tanzania haijafanya juhudi za kupambana na ujangili wa meno ya tembo, akisema taarifa hizo ni uzushi na upuuzi mtupu.
 Wakati kuna joto la vyombo vya habari vya kimataifa kuituhumu Tanzania kuwa haipambani na ujangili, Rais Jakaya Kikwete amesema Serikali imeubaini mtandao unaojumuisha watu 40, akiwemo tajiri maarufu mkoani Arusha.
Akihojiwa juzi jioni na Idhaa ya Kiswahili ya BBC, Rais Kikwete alikanusha taarifa zilizotolewa na gazeti la Sunday Mail la Uingereza zilizodai Tanzania haijafanya juhudi za kupambana na ujangili wa meno ya tembo, akisema taarifa hizo ni uzushi na upuuzi mtupu.
“Gazeti hilo limezungumza na nani, ndiyo maana sitaki kupoteza muda kujadili upuuzi, achana na mambo hayo. Ndiyo maana tunasema, akutukanaye hakuchagulii tusi,” alisema Rais Kikwete.
Alisema inashangaza kuona watu wanaozusha taarifa hizo hawaoni jinsi tulivyofanya jitihada za kutokomeza ujangili, kama operesheni za tokomeza ujangili na operesheni kipepeo.
Kuhusu majangili 40 ambao wametambuliwa, Rais Kikwete alisema wameutambua mtandao mkubwa wa majangili unaoongozwa na mfanyabiashara mkubwa wa Arusha Mjini.
“Kuna majangili 40 waliotambuliwa na tumetambua mtandao mzima, pale Arusha kuna mtu mkubwa alikuwa anaendesha biashara. Kazi ilikuwa ni kutambua mtandano wote, ule mtandao ni mpana sana,” alisema Rais Kikwete.
Katika mahojiano hayo, Rais Kikwete alisema, Tanzania ilikuwa ni nchi yenye tembo wengi zaidi duniani, lakini ujangili ulipokithiri, tembo walipungua na kufikia 57,000 tu mwaka 1987.
“Mwaka 1989, Taasisi ya Kimataifa ya Cites, walipiga marufuku biashara ya meno ya tembo duniani na ujangili ulipungua kwa kiasi kikubwa hivyo tembo waliongezeka na kufikia, 110,000 mwaka 2009,” alisema.
Kikwete ahojiwa CNN
Rais Jakaya Kikwete amekiri kuwa vita dhidi ya ujangili ni tatizo sugu linaloielemea Tanzania.
Wakati idadi ya tembo ikiendelea kupukutika kila siku, vita dhidi ya ujangili ilichukua sura mpya mwishoni mwa mwaka jana baada ya operesheni iliyofahamika kwa jila la Tokomeza Ujangili, kukumbwa na kashfa ya ukiukwaji wa haki za binadamu na kusababisha mawaziri wanne kujiuzulu.
Mawaziri waliojiuzulu ni pamoja na aliyekuwa Waziri wa Maliasili na Utalii, Balozi Khamis Kagasheki, aliyekuwa Waziri wa Mambo ya Ndani ya Nchi, Dk Emmanuel Nchimbi, aliyekuwa Waziri wa Ulinzi na Jeshi la Kujenga Taifa, Shamsi Vuai Nahodha na aliyekuwa Waziri wa Mifugo na Uvuvi, Dk David