Showing posts with label wasanii. Show all posts
Showing posts with label wasanii. Show all posts

Saturday, 22 February 2014

DIAMOND KUHUDHURIA TUZO ZA 'AFRIMMA' ZITAKAZOFANYIKA TEXAS MAREKANI, ZITAHUSISHA WASANII WAKUBWA AFRIKA..



July 26 mwaka huu, wasanii wengi wakubwa Afrika kutoka katika mataifa ya 17 watakutana Dallas, Texas, Marekani kuhudhuria utoaji wa tuzo za kiafrika zinazojulikana kama ‘AFRIMMA Awards’, na tayari Diamond Platinumz tayari ameshaonesha uthibitisho wa kuwa katika daftari la mahudhurio siku hiyo.
 
Diamond amepost kwenye Instagram video inayomuonesha akifanya promo maalum iliyoandaliwa na watayarishaji akiwaambia mashabiki kwa swag za kimarekani kuwa atakuwepo siku hiyo, na kisha akaisindikiza na maneno yanayosomeka, “Yess! i'll be ryt there....Afrimma Awards 26/07/2014 Texas, Dallas (USA).”
 
Tuzo hizo zilizoandaliwa na Big A Entertainment na African Muzik Magazine, zimelenga katika kuwatunuku wasanii mbalimbali wakubwa wa Afrika waliopo duniani kote na itagusa nyanja mbalimbali za burudani ikiwa ni pamoja na wasanii wa muziki, wachezea santuri aka Dj’s, watayarishaji wa muziki, mameneja na watu wanaousapoti utamaduni wa Afrika.
 
Tuzo hizo zinatarajiwa kusindikizwa na vicheko vya mara kwa mara kwa kuwa mshereheshaji wa shughuli hiyo ni mchekeshaji maarufu wa kimataifa, The Basket Mouth na atakuwa na muigizaji mrembo wa Nollywood, Juliet Ibrahim.

Friday, 21 February 2014

ABU KIBA AFUNGUKA SABABU ZA KAKA YAKE "ALI KIBA" KUWA KIMYAA..SOMA HAPA KUZIJUA

 
Ali Kiba, mwimbaji aliyewahi hutajwa na mfalme wa R&B duniani Robert Kelly kama mmoja kati wa wasanii wenye sauti poa zaidi katika mradi wa One 8 amekuwa kimya kwa kipindi cha mwaka mmoja, huku wengi wakitoa sababu kadhaa za kufikirika kuhusu ukimya wake.
Tovuti ya Times Fm imeongea na ndugu wa damu wa Ali Kiba, Abul Kiba ambaye mbali na kuwa msanii aliyetambulishwa kwenye game na kaka yake, amekuwa akisaidia kuzifuatilia na kuzisimamia kazi zake.
Abdu Kiba ameeleza kuwa ukimya wa ndugu yake unatokana na kubanwa na majukumu ya kifamilia.
“Unajua watu wengi wanahisi vibaya sana, mara mwingine anaibuka na kusema amefulia kwenye game,sio kweli naomba niweke sawa kuhusu suala hili ni kwamba Ally Kiba alikuwa na majukumu ya kifamilia pamoja na kazi zake,maana nakumbuka tangu anitambulishe kwenye muziki wa Bongo Flava ndio alianza kubanwa na mambo  yake binafsi.” Amesema Abdu Kiba.
Hata hivyo, mashabiki wa Ali Kiba wana kila sababu ya kukaa mkao wa kusikia hits za mkali huyo mwaka huu.
“Niliwahi kuzungumza nae hivi karibuni, akaniambia mwaka huu anatarajia kuja kivingine katika game. Kwa sasa anajaribu kumalizia baadhi ya nyimbo alizorekodi ili mwaka huu mashabiki wazisikie katika vituo mbalimbali vya radio.” Abdu Kiba aliieleza

Wednesday, 19 February 2014

Dully Sykes Afunguka mara baada ya Video ya Nyimbo yake ya ‘Kabinti Spesho’ Kupigwa Marufuku na Serikali.

DULLY1
Baada ya ngoma yake ya Kabinti Spesho ya Staa wa Bongo Fleva,Dully Sykes kufungiwa na serikali kutopingwa kwenye vituo vya televisheni,kutokana na kutokuwa na maadili ya Kitanzania,amesema amekata tamaa ya kuwa msanii wa Kimataifa kutokanana kitendo hicho kumvunja moyo.Kwa mujibu wa msanii huyo amesema hiyo imetokana na serikali kupitia mamlaka ya mawasiliano TCRA kutoa onyo kwa vituo vya televisheni zisiipige video hiyo kutokana na kuvunja maadili hasa maandishi yaliyopo kwenye t-shirt aliyovaa msanii Diamond Platinumz, pili ni ile swimming costume aliyovaa video queen.

Video nyingine zilizopigwa stop ni pamoja na Uzuri Wako ya Jux, na Nimevurugwa ya Snura.

Tuesday, 18 February 2014

DIAMOND NI NOMAAAAA..!! TAZAMA JISI ALIVYOMFUNDISHA D'BANJI KUCHEZA NGOLOLO AKIWA SOUTH AFRICA

PICHA MBALI MBALI NIKIWA NA D-BANJ NCHINI SOUTH AFRICA

 Ngololo master pale coco master....!!!

 Babu Tale,Salam na Dbanj
Interview Redion nikiwa na Vic.kiman wa Kenya na Dbanj


AY, MWANA FA NA DIAMOND WAUNGANA NA WASANII ZAIDI YA 19 AFRIKA KUFANYA WIMBO MMOJA AFRIKA KUSINI -

Wasanii kutoka Tanzania, Ambwene Yessaya na Diamond Platnumz siku ya jana walisafiri kuelekea Afrika Kusini ambako wanaungana na wasanii wengine kutoka bara la Afrika kwa ajili ya kufanya wimbo wa pamoja ambao unatambulika kama mradi wa “Do Agric” kwa ajili ya kuhamasisha kilimo barani Afrika huku ikitumika kuwashtua viongozi wa Afrika juu ya kuchangia asilimia kumi kwenye kilimo.

 

Juma Nature Akana Madai ya Kumponda Diamond kwenye Nyimbo yake Mpya…Adai ‘Dada Mondi’ ni Msanii tofauti.

nature
Hatimaye Juma Nature, amezungumzia utata ulioibuka kwenye wimbo wake mpya Kama Jana, unaohusiana na kama kweli amemdiss Diamond.
Akiongea na kipindi cha Showtime Next Chapter, Juma Nature aka Kiroboto amesema jina la ‘Dada Mondi’ lililofanya wengi waamini kuwa ni version yake ya Diamond, ni jina la msanii mwingine kabisa.
“Hamna diss ya kumdiss Diamond, Diamond hajadisiwa,” amesema Nature.
“Pale katajwa mtu mwingine kabisa anaitwa Dada Mondi na anakaa mitaa ya kwetu. Bado hajatoka halafu anataka sifa.”
nature

NATURE ATUPIWA MANENO MAKALI BAADA YA KUMDISS DIAMOND KWENYE WIMBO WAKE MPYAAA.....SOMA COMMENT ZAO HAPA


Wimbo mpya wa Juma Nature ‘Kama Jana’ umezusha mjadala kwa mashabiki na wengi wameonesha kutopenda kitendo chake cha kumdiss Diamond kwenye wimbo huo. Juma Nature
Katika wimbo huo aliomshirikisha Lady Jaydee, Nature anasema: ‘Usiwe limbukeni wewe Dada Mondi, wakikuita mashabiki unakula bundi’ Kukata kiuno sana kwani ndio ufundi?
Haya ni baadhi ya maoni ya wasomaji wa Bongo5.
Anthony Kuhama
Ms**ge tu mziki ushamfunga pingu wanatafuta njia ya kuludi kwa kudis aaaaaah kweli upepo wa diamond kiboko mnaishia kuuza ndala na t shirt za home sweet home. aaaaah

Gara B Kubwa

Wala hakuna haja ya kumtusi Nature..yeye kauliza Swali akimtolea Dai kama Mfano..JIbu la Swali lake la “Kwanini Bongo Fleva isifanywe kama jana?” ni hivi.. “Leo sio Kama Jana.coz ata hyo jana anayotaka yeye ilikua na Juzi na mziki ,mbona yeye hakufanya mziki wa juzi? Hivo ata kesho na keshokutwa mziki utabadilika tu..Nmesikitika tu LadyJaydee kuitikia Chorus nzuri kwny hii nyimbo mbovu ya Mkubwa Nature.

Junior Kisaka Stunna

Inamana nature naye keshaishiwa vya kuimba hadi anmdiss diamond ili apate kick? cuz tushazoea kuwa mtu akimdiss diamond bac lazma apate kick tu, ajiulize diamond sahiv yuko wapi? kwa hapo nature umechemka tulikuwa tunakuheshimu lakin umechemka bro. mziki hauendi hivyo ndio mana hamuendelei sasa nyimbo kama hiyo itafika wapi? zaidi ya kuishia bongo tu? damnnnnnnn.
Siza Shitindi
Ckutegemea kama Juma nature na heshima yako utaimba upumbavu namna hiyo,nyimbo mbovu au unatafuta kick yakutokea kupitia Diamond,we uza mitumba tu maana umeonyesha dhahiri kwamba huna jipya kabixaa mzik umekupg pingu kakaaa

Mwalimu Kaijage

Kwanini wasanii wa Kibongo,wanapenda sana bivu? kwani ni lazima amtaje Diamond ktk wimbo wake.
Ibrahimu Abedi
Kakosa maneno yakuandika aache us**ge hata kama mkongwe
Goodluck Lwaho
Mi naona hajamtusi ila kaimba kitu ambacho kipo

DIAMOND NA D'BANJI NDANI YA STUDIO WAKIANDAA KITU KIPYAAAA..JIONEE PICHA HAPA







Picha ni Diamond Platnumz na D' BANJ wakiwa studio ready kutengeneza muziki mpya, sasa Diamond kutoa nyimbo nyingine na D'BANJ..Diamond alipost hiyo picha na kuandika maneno haya hapa chini..

Monday, 17 February 2014

MANAIKI SANGA NA NEY WA MITEGO SASA NI KAMA PAKA NA PANYA STI MANAIKI AME...... NA DEMU WA NEY ,,SOMA HAPA KUJUA UKWELI



 Msanii wa Bongo Movie nchini Manaiki Sanga "The Don" 
Mwanamuziki wa bongo Flava Nay wa Mitego akiwa na mchumbaake aliyezusha balaa baada ya Manaiki Sanga kudai kuwa keshampitia na kutaja alama zilizopo mwilini mwake.

Na Mwandishi Wetu
Msanii Manaiki Sanga "The Don" ameonekana kumtafuta Ney wa Mitego na kuingilia ndoa yake baada ya kuandika kwenye mtandao wa Facebook akisema kuwa mke anaejitambia Nay ameshamla uloda sana kiasi cha kutaka kumuoa.
Kwenye post hiyo Manaiki alisema kuwa msichana huyo ambae hakumtaja jina alikuwa kama mke wake kwa kipindi kirefu sana na hadia nakuja kumchukua Nay ambae hivi karibuni ametangaza kumnunulia gari la milini therathini kama zawadi.

AY, DIAMOND Waelekea Sauzi Kwenye Kampeni za kuhamasisha Kilimo.

diamond
Mastaa wa Bongo Fleva,AY na Diamond wameelekea nchini South Africa kujiunga na wasanii wengine zaidi ya kumi kutoka pembe zote za Africa kwa ajili ya kusapoti na kurekodi ngoma kuhamasisha vita dhidi ya umaskini na njaa kwa kutumia kilimo.
ONE ni kampeni ambayo ilianzishwa na msanii kutoka kundi la U2 anaitwa Bono 2004 na ameshachangisha mamilion ya dola kwa ajili ya kusaidia maskini na matajiri mbalimbali huchangia project hiyo akiwemo Bilionea Bill Gates na mkewe Melinda Gates.
Mwaka jana kulikuwa na malalamiko kwanini kampeni hii haina sauti ya Waafrika kwasababu wao ndo maskini wenyewe, kiuchumi.
Ndiyo sababu mwaka huu wasanii kutoka barani Afrika wamepata nafasi ya kutoa kilio chao.
Leo AY na Diamond Platinum wameelekea nchini South Africa kubariki mradi huo.

TAZAMA PICHA ZASHOW YA OMMY DIMPOZ ALIYOFANYA LONDON SIKU YA VALENTINE