July 26 mwaka huu, wasanii wengi wakubwa Afrika kutoka katika mataifa ya 17 watakutana Dallas, Texas, Marekani kuhudhuria utoaji wa tuzo za kiafrika zinazojulikana kama ‘AFRIMMA Awards’, na tayari Diamond Platinumz tayari ameshaonesha uthibitisho wa kuwa katika daftari la mahudhurio siku hiyo.
Diamond
amepost kwenye Instagram video inayomuonesha akifanya promo maalum
iliyoandaliwa na watayarishaji akiwaambia mashabiki kwa swag za
kimarekani kuwa atakuwepo siku hiyo, na kisha akaisindikiza na maneno
yanayosomeka, “Yess! i'll be ryt there....Afrimma Awards 26/07/2014
Texas, Dallas (USA).”
Tuzo
hizo zilizoandaliwa na Big A Entertainment na African Muzik Magazine,
zimelenga katika kuwatunuku wasanii mbalimbali wakubwa wa Afrika waliopo
duniani kote na itagusa nyanja mbalimbali za burudani ikiwa ni pamoja
na wasanii wa muziki, wachezea santuri aka Dj’s, watayarishaji wa
muziki, mameneja na watu wanaousapoti utamaduni wa Afrika.
Tuzo
hizo zinatarajiwa kusindikizwa na vicheko vya mara kwa mara kwa kuwa
mshereheshaji wa shughuli hiyo ni mchekeshaji maarufu wa kimataifa, The
Basket Mouth na atakuwa na muigizaji mrembo wa Nollywood, Juliet
Ibrahim.
0 comments:
Post a Comment