Showing posts with label kimataifa. Show all posts
Showing posts with label kimataifa. Show all posts

Tuesday, 18 February 2014

Waziri mkuu Italia radhi kuondoka,,,,,,,,,,,,,kwa nini? Soma hapa kujua sababu,,,,,,,,,,,



Enrico Letta
Rais wa Italia, Giorgio Napolitano, amepokea barua ya kujiuzulu kwa waziri mkuu, Enrico Letta. Letta aliiwasilisha rasmi barua hiyo siku moja baada ya chama chake kupiga kura kujitoa kwenye muungano wa utawala.
Wandani wake katika chama chake cha Democratic ndio waliomfuta kazi. Hatua hiyo iliunga mkono changamoto dhidi ya Letta kutoka kwa kinara mpya ambaye ni kijana mwenye maono Matteo Renzi.
Kitakacho fanyika sasa kimo mikononi mwa rais wa Italia, Napolitano.
Hata hivyo kuna uwezekano mkubwa wa rais huyo kumchagua Bw. Renzi kuwa waziri mkuu kisha aunde serikali.
Hicho kitakuwa kilele cha safari ya uongozi wake. Bw.Renzi aliye na umri wa miaka thelathini na tisa, hajawahi kuchaguliwa bungeni, wala kuitumikia serikali. Ni wazi kwamba hana uzoefu lakini ni analeta matumaini ya kuleta mageuzi.

Serikali ya Syria yaingia lawamani


Wajumbe katika mkutano wa amani wa Geneva.
Mataifa ya Ufaransa na Uingereza yameilaumu Serikali ya Syria kwa kuanguka kwa mazungumzo kati yake na upinzani mjini Geneva.
waziri wa maswala ya kigeni nchini Ufaransa amesema kuwa wajumbe wa rais Assad walipinga mipango yote ya kubuni serikali ya mpito.
Mpatanishi mkuu wa umoja wa mataifa Lakhdar Brahimi aliomba msamaha kwa raia wa Syria kwa tukio hilo.
Amesema alishindwa kubuni tarehe nyengine ya mazungumzo,huku akitoa matumaini kwamba vikao hivyo vitalazimika kuendelea katika siku za usoni.
Wanaharakati wanasema kuwa takriban raia elfu sita wa Syria wameuawa tangia awamu ya kwanza ya mazungumzo hayo ianze mwezi uliopita.