09:30
No Comments
Wafanyakazi wa kampuni ya Strabag,
inayojenga barabara ya mabasi yaendayo kasi, wakimdhibiti kijana
aliyetuhumiwa kuiba vifaa vya ujenzi wa miundombinu ya barabara na
kukwamisha kwa muda maendeleo ya ujenzi huo katika eneo la Magomeni
Kagera jijini Dar es salaam.
Hata hivyo, kundi la vijana
wanaodhaniwa kuwa vibaka wenziye, walifanikiwa kumkomboa kijana huyo
kabla ya kufikishwa kwenye mikono ya sheria, baada ya kutokea tafrani
kubwa kati ya wahuni hao na wafanyakazi wa Strabag waliopewa dhamana ya
ujenzi huo na serikali ya Jamhuri ya Muungano ya Tanzania, chini ya
wizara ya ujenzi inayoongozwa na Mh. Magufuri.
Katika tukio hilo, mmoja wa
wafanyakazi wa Strabag (aliyemshika kijana huyo, Pichani) alijeruhiwa
vibaya kwa mawe kutoka kwa wahuni hao wakati wa harakati hizo za
kumkomboa mwenzao ambaye walitokomea naye vichochoroni huku bado akiwa
amefungwa kamba.
Angalia Picha zaidi
0 comments:
Post a Comment