Monday, 17 February 2014

AY, DIAMOND Waelekea Sauzi Kwenye Kampeni za kuhamasisha Kilimo.

diamond
Mastaa wa Bongo Fleva,AY na Diamond wameelekea nchini South Africa kujiunga na wasanii wengine zaidi ya kumi kutoka pembe zote za Africa kwa ajili ya kusapoti na kurekodi ngoma kuhamasisha vita dhidi ya umaskini na njaa kwa kutumia kilimo.
ONE ni kampeni ambayo ilianzishwa na msanii kutoka kundi la U2 anaitwa Bono 2004 na ameshachangisha mamilion ya dola kwa ajili ya kusaidia maskini na matajiri mbalimbali huchangia project hiyo akiwemo Bilionea Bill Gates na mkewe Melinda Gates.
Mwaka jana kulikuwa na malalamiko kwanini kampeni hii haina sauti ya Waafrika kwasababu wao ndo maskini wenyewe, kiuchumi.
Ndiyo sababu mwaka huu wasanii kutoka barani Afrika wamepata nafasi ya kutoa kilio chao.
Leo AY na Diamond Platinum wameelekea nchini South Africa kubariki mradi huo.

0 comments:

Post a Comment