Lori la mafuta limeanguka jioni hii katika eneo la milima ya
sekenke mkoani Singida na kuua watu wanne hapohapo.Chanzo cha ajali hiyo
ni breki kufeli kukamata wakati lori hilo lilipokuwa linashuka mlima
huo.Shuhuda wa ajali hiyo bwana Julius Chacha alipoongea na mtandao wetu
wa Dj sek blog amesema kwamba Lori hilo lilipoacha njia lilipinduka na
kuingia bondeni na kushika moto.Akiendelea kuongea shuhuda huyo alisema
walishindwa kutoa msaada wowote kwa kuwa moto uliposhika ulikuwa mkubwa
na hawakuwa na vifaa vya kuokolea.Watu wanne wamekufa papo hapo kutokana
na ajali hiyo.Polisi walikuwa bado hawajafika eneoo la tukio mpaka
tunaondoka eneo la tukio.
Baadhi ya Wananchi waliofika katika
ajali hiyo wakiangalia mabaki ya Lori hilo baada ya kupata ajali na
kuwaka moto leojioni likiwa katika safari zake za kusafirisha Mafyta nje
ya Dar-es-Salaam, kupeleka mkoa wa jirani..
Mabaki ya Lori hilo baada ya kuteketea kabisa na moto jioni hii, baada ya kupata ajali katika eneo la mlima sekenke.
Baadhi ya wasafiri wakitazama lori lililongua jioni hii
Bonde la mlima sekenke linavyoonekana na baadhi ya miti imeunguaa
Hii ni njia ya mlima sekenke
0 comments:
Post a Comment