Showing posts with label siasa. Show all posts
Showing posts with label siasa. Show all posts

Friday, 21 February 2014

Alichokisema Zitto mara baada ya Wajumbe wa Bunge la Katiba Kudai Nyongeza ya Posho na kudai kuwa Tshs. 300,000/= kwa Siku Haiwatoshi.

zito Ishu ya posho za bunge la katiba ndiyo inayoongelewa sana hivi sasa ambapo pamoja na headlines zote za Wabunge, haya ni mawazo ya Mbunge wa Kigoma Kaskazini Zitto Kabwe kuhusu hii posho.
“Naomba niseme wazi kabisa kwamba, sitapokea nyongeza yeyote ya posho hata ikiongezwa. Inaweza isisaidie kuzuia walafi wengine kupata posho kubwa lakini ni bora kuhesabika kwamba nimesema hapana. Ifikie wakati tuseme hapana kwa excesses zisizo na maana. Ninamwomba Rais asikubali kuongeza posho kama baadhi ya wajumbe wa BM wanavyotaka. Wanachopata kinawatosha sana. Nawasihi wananchi mumwombe na ikibidi kumshinikiza Rais kukataa.”

Tuesday, 18 February 2014

PANDU AMIR KIFICHO AIBUKA KIDEDEA MWENYEKITI WA MUDA WA BUNGE MAALUMU LA KATIBA


Spika wa Bunge la Wawakilishi Zanzibar, na Mbunge wa Bunge maalum la Katiba, Pandu Amir Kificho (Pichani kushoto) akisalimiana na Makamu wa Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, wakati walipokutana katika sherehe za Muungano mjini Zanzibar hivi karibuni. 
Kificho ameibuka kidedea kwa kuchaguliwa kuwa Mwenyekiti wa muda wa Bunge Maalumu la Katiba, baada ya kuwamwaga wapinzani wake kwa jumla ya kura 393, huku wapinzani wake Magdalena Rwebangira na Mahalu, wakifungana kwa kupata kura 84 kila mmoja.

“NILIWAHI KULIPWA MIL 10 KWA KUFANYA SHOW MOJA YA MUZIKI MSIFIKIRI DIAMOND NDIO WA KWANZA”….MB DOG

mbdog
Kama ulifikiri bongo fleva ilianza kulipa mamilioni miaka ya akina Diamond Platinumz, Ommy Dimpoz na wengine, nikimaanisha kuanzia mwaka ya 2010, kwa leo inabidi ubadili mawazo yako.

“Lakini uzuri wakati mimi naanza kufanya, kazi zilifanyika na misingi za ile kazi zilikuwa zimekaa tofauti na watu wanavyosikia. Kwa hiyo uoga hata wa mapromota ulikuwepo wakati wanatusogelea. Kwa hiyo hatukuwa tunalipwa laki tatu viiile.” Mbwana Mohammed aka MB Dog ameiambia tovuti ya Times Fm.

Huenda inawezekana ulikuwa hujui kwa sababu wakongwe waliokuwa wanahit enzi hizo hawakuwa na tabia ya kuweka wazi kiasi wanacholipwa kama wanavyofanya wakali wa bongo flava wa kizazi hiki cha dijiti.

Mkali huyo wa ‘Latifa’ ameiambia tovuti ya Times Fm kuwa alikuwa anakutana na milioni kadhaa kwenye show zake, na kwamba kiasi kikubwa zaidi alichowahi kulipwa kilikuwa shilingi milioni kumi nchini Burundi.

“Yaani mimi show ya kwanza nimeanza kuifanya nimelipwa milioni tatu, show ya mwisho mimi kuifanya nimelipwa milioni kumi…ambayo ndiyo ilikuwa show ya maajabu yaani…kwa ubongo wangu  nawaza naweza kufanya show tena ya watu wengi kama wale!! Nadhani ilikuwa mwaka 2006.” Amesema MB Dog na kusisitiza, “milioni kumi za kitanzania”.
mbdog

Kumbe Bongo Flava ilianza kulipa zamani japo kwa wachache! Na huenda ni kwa sababu tu watu walikuwa hawaweki wazi wanachoingiza.

Hapa tumpigie picha Mr. Nice wa enzi hizo kwa kutumia mfano wa MB Dog.

Kama kweli mambo yalikuwa hivi, inaweza kuwa moja kati ya sababu zilizozaa wazo kati ya wakongwe Juma Nature na Lady Jay Dee kutaka Leo iwe ‘Kama Jana’.

MBOWE AZIMA VURUGU BUNGE LA KATIBA, KURA ZARUDIWA KUHESABIWA..!!

mbowe
MWENYEKITI wa Chama Cha Demokrasia na Maendeleo (Chadema),Freeman Mbowe ameonyesha ukomavu mkubwa katika uongozi na masuala ya siasa baada ya kufanikiwa kumwongoza Mwenyekiti wa Bunge maalum la kumtafuta Mwenyekiti wa muda wa Bunge hilo.
Mwenyekiti wa Bunge hilo Oliva Luena alikubwa na wakati mgumu wa kuliongoza bunge hilo, lenye wajumbe zaidi ya 548,katika mchakato wa kumtafuta mwenyekiti wa muda,hali ilikuwa tete ndani ya ukumbi huo wa bunge baada ya kura kuharibika kutokana wajumbe zaidi 45 kuongezeka, badala ya wajumbe 548 waliokuwepo wakati wa zoezi la kupiga kura.

Hatua hiyo ilimlazimu Mwenyekiti huyo kuamuru zoezi la upigaji kura urudiwe,huku baadhi ya wajumbe wa bunge hilo maalum wakipinga hatua hiyo kwa madai kwamba itapoteza muda na pengine wakaja kurudia tena zoezi hilo.

Wajumbe hao waliokuwa wakizungumza bila kufuata utaratibu, huku wakishindwa kumsikiliza Mwenyekiti wao Luena kutokana na kile walichodai kwamba kura zilizozidi ziondolewe,huku wengine wakidai kwamba kila mjumbe ahesabiwe kwa mtindo wa namba moja hadi mwisho yaani kila mmoja asema namba moja hadi wa mwisho.

Hata hivyo hali hiyo ilimfanya Mbowe asimame na kuzungumza kwa hekma na busara huku akimtaka Mwenyekiti huyo kufuata ushauri wake, ambapo alisema kwamba,  ”Mwenyekiti naomba utumie hekma kurudia zoezi la kura kupigwa upya”, kauli ambayo ilipingwa na baadhi ya wajumbe.

Mbali na kupingwa vikali na baadhi ya wajumbe waliokuwa ndani ya ukumbi huo wa bunge, huku mjumbe mmoja akizungumza ovyo na kusema kwamba kila mmoja asimame nyuma ya mgombea anayempenda ndipo wahesabiwe.

Wajumbe hao pia hawakuzingatia hata heshma ya kiti aliyokalia mwenyekiti Oliva Luena kuwapa nafasi, Mbowe bado hakutaka kutumia jazba badala yake akaendelea kusisitiza kwa kauli ya upole,hekma na busara kumuomba mwenyekiti huyo kukubali ushauri wake wa kura kudiwa.

Mbowe alisema,”Mwenyekiti mimi nina mambo matatu ya kukushauri katika zoezi hili, moja milango yote ifungwe ili watu wasiokuwepo huku ndani wasiingie kuvuruga uchaguzi huu,pili wajumbe wote wakae chini,tatu karatasi za kupigia kura,zigawiwe kwa kila mjumbe kwa kupelekewa kwenye kiti chache, kwani kwakufanya hivi tutakuwa tumekwepa historia mbaya ya kura kurudiwa ndani ya nchi hii”.Hatimaye Mwenyekiti wa bunge la mpito Oliva Luena alikubaliana na ushauri huo na kuamuru zoezi la upigaji kura urudiwe. Wagombea waliokuwa wakipigiwa kura ni pamoja na Pandu Ameir Kificho ,Magdalena

Mbatia, Mbowe Wageuka Mbogo kuhusu Kauli ya Rais Kikwete..!!

mbatia
Kauli ya Rais Jakaya Kikwete ya kuwataka wanachama, wadau na makada wa CCM, kuondokana na unyonge, imepokewa kwa hisia tofauti huku ikielezwa kuwa ni ya vitisho.

Juzi, wakati akifungua Mkutano wa Halmashauri Kuu ya CCM mjini Dodoma, Rais Kikwete ambaye pia ni Mwenyekiti wa chama hicho tawala alisema: “Ni wakati wa kuacha unyonge na uvumilivu una kikomo chake.”

Alisema CCM inaingia kwenye uchaguzi huku ikishindana na wagomvi: “…Ugomvi ndiyo sehemu ya mwongozo wao kufanya siasa,” alisema Kikwete bila kutaja jina la chama chochote cha siasa.

Alisema amechoshwa na vitendo vya ugomvi huku akitolea mfano wa tukio la Kahama mkoani Shinyanga ambako kijana mmoja alitolewa macho kwa bisibisi na mwingine kumwagiwa tindikali katika uchaguzi mdogo wa ubunge Igunga, mkoani Tabora.

Akizungumza kwa simu jana, Mwenyekiti wa Chadema, Freeman Mbowe alieleza kushangazwa kwake na kauli ya Rais Kikwete akisema: “Nimeipokea kwa mshtuko na ninawataka wafuasi wa chama changu kuwa watulivu na kuchukua tahadhari kubwa.”

“Nilichokifanya ni kuwaagiza wafuasi wa Chadema kufanya kampeni za kistaarabu kwa kutolipiza kisasi ili kuhakikisha kwamba hakuna damu ya Mtanzania itakayomwagika Kalenga,” alisema.

Hatua ya Rais Kikwete, imekuja baada ya CCM kumtangaza, Godfrey Mgimwa kuwa mgombea ubunge wa Jimbo la Kalenga. Mgimwa ni mtoto wa aliyekuwa mbunge wa jimbo hilo, ambaye pia alikuwa Waziri wa Fedha, hayati Dk William Mgimwa aliyefariki mwezi uliopita nchini Afrika Kusini.

Mgombea huyo atachuana na mgombea wa Chadema, Grace Tengega.

Jana, Mbowe alisema ingawa Kikwete ni Mwenyekiti wa CCM, alitakiwa kufahamu kwamba ni kiongozi wa nchi na ni Amiri Jeshi Mkuu ambaye vikosi vya Ulinzi na Usalama vipo chini yake.
mbatia“Anapotoa kauli nzito kama hiyo, inatakiwa afahamu kwamba yeye si Mwenyekiti wa CCM tu, bali ni Rais na Amiri Jeshi Mkuu, hakustahili kutoa kauli kama hiyo inayoweza kuamsha hisia,” alisema Mbowe.

Alisema kauli zake za kiitikadi za kupendelea chama chake wakati akifahamu kuwa yeye ni kiongozi wa Watanzania wote, zinawafanya wananchi wagawanyike kwa misingi ya vyama.

“Rais Kikwete anadai kwamba mtu wao alimwagiwa tindikali na mwingine kutolewa macho kwa bisibisi, lakini hazungumzii viongozi na wanachama wa Chadema waliouawa kwa kupigwa risasi na wengine kwa mabomu. Anasema hayo huku akifahamu fika kwamba kuna vyombo vya dola na Mahakama ambavyo vinashughulikia matukio hayo.”

Urais 2015 ndani ya CCM hali si shwari


HARAKATI za kuwania urais mwaka 2015 ndani ya Chama cha Mapinduzi (CCM), zimefika hatua mbaya ya watu wanaotajwa kuwa katika orodha ya wagombea na wapambe wao kuingiwa na hofu ya kudhuriana na kuombeana mabaya,
Hofu hiyo imeongezeka zaidi hasa kutokana na ugonjwa wa ajabu anaougua Naibu Waziri wa Ujenzi, Dk. Harrison Mwakyembe, ambao taarifa zisizo rasmi zinauhusisha na kuwapo kwa mikono ya watu.
Ingawa hadi sasa si Mwakyembe mwenyewe au mamlaka yoyote ya umma aliyetoa taarifa rasmi ya nini hasa anaugua mwanasiasa huyo, lakini kauli ambazo alizitoa siku chache zilizopita zinaongeza chumvi katika mashaka hayo.
Akizungumza na waandishi wa habari hivi karibuni, Mwakyembe aliyerejea kutoka katika matibabu nchini India alisema hana sababu ya kulipiza kisasi na kwamba anamwachia Mungu.
Kauli hiyo imeibua maneno mengi miongoni mwa wanasiasa ambao baadhi wamekuwa wakiitafsiri kuwa inayothibitisha wasiwasi uliotanda kwamba huenda mwanasiasa huyo anaugua kutokana na kudhuriwa na wanasiasa washindani wake.

Wakati ugonjwa anaougua Mwakyembe ukiwa bado unazusha mashaka, kuugua kwa muda mrefu kwa Waziri wa Maji na Umwagiliaji, Profesa Mark Mwandosya nako kuliibua maneno mengi.
Habari ambazo zilimkariri Mwandosya mwenyewe na watu walio karibu naye zinaeleza kwamba, ugonjwa wake ulisababisha baadhi ya wanasiasa ndani ya CCM kumchulia kifo kutokana na maradhi hayo.
Kabla na baada ya kurejea nchini kutoka katika matibabu yake nchini India, Mwandosya alikaririwa akisema watu waliokuwa wakimchulia kifo, walitakiwa kutambua kwamba watalazimika kusubiri kwa muda mrefu kabla ya hilo (kifo) kumfika.
Wakati hali ikiwa hivyo, uchunguzi uliofanywa na gazeti hili, umebaini kuwa, kumekuwa na hali ya kutoaminiana na kutiliana sana mashaka miongoni mwa makada maarufu ndani ya CCM ambayo yote inahusishwa na mchakato wa urais ndani ya chama hicho mwaka 2015.
Kada mmoja maarufu wa CCM aliyezungumza na Tanzania Daima Jumatano amesema wamefikia hatua ya kujilinda kwa kuwa waangalifu katika matembezi na sehemu wanazokula chakula kwa sababu hizo hizo.
Kwa mujibu wa kada huyo, wanasiasa takriban wote wanaotajwa kuwa wanatarajia kugombea urais kupitia chama hicho wamefikia hatua ya kujilinda kwa silaha za moto na wengine kutumia mafuta maalum yanayoaminika kuzuia sumu.
“Tumefika pabaya, hali ni ngumu sana. Sasa hivi watu wamegawana hata maeneo ya kutembelea. Kwa mfano kama kundi fulani lina kawaida ya kupata bia kwenye baa au hoteli fulani, makada wa kundi lingine hawafiki.
“Ikitokea mmekutana kwa bahati mbaya, mmoja lazima aondoke,” alisema mmoja wa makada wanaotajwa kuwania urais.
Kiongozi mmoja mstaafu anayetajwa kuwa miongoni mwa wagombea urais naye anaelezwa kwamba amelazimika kuchukua hatua kadha wa kadha za kujilinda ili kuepukana na hatari ya kudhuriwa na washindani wake wa kisiasa ndani ya CCM.
“Hivi sasa tumefika mahali tunasafiri kwa tahadhari kubwa na kwa kutumia usafiri ambao baadhi ya watu wanaotulenga hawawezi kututambua kama njia ya kukabiliana na hatari ambayo inahusishwa na urais wa mwaka 2015,” amekaririwa akisema mwanasiasa huyo mstaafu.
Wakati hayo yakitokea kumbukumbu zinaonyesha kwamba kwa nyakati tofauti wanasiasa wawili, akiwamo Mwakyembe mwenyewe na Waziri wa Ushirikiano wa Afrika Mashariki, Samuel Sitta wamepata kutoa taarifa za maisha yao kutishiwa.
Sitta ambaye duru za kisiasa zinamtaja kuwa mmoja wa wanaofikiria urais, amepata kukaririwa kwamba amekuwa akipokea vitisho vya kuuawa kupitia simu yake ya mkononi kwa njia ya ujumbe mfupi na watu asiowajua.
Mgombea mwingine ambaye jina lake nalo limehusishwa na tishio la maisha yake ni Waziri Mkuu wa zamani, Edward Lowassa.
Gazeti moja la kila wiki (siyo Tanzania Daima) lilipata kumkariri mtoto wa mwanasiasa huyo akilalamika kuhusu kuwapo kwa tishio la maisha ya mzazi wake huyo.
Ingawa wenyewe hawajatamka rasmi, baadhi ya makada wengine wanaotajwa kufukuzana kurithi nafasi ya Rais Jakaya Kikwete mwaka 2015 ni pamoja na Waziri wa Mambo ya Nje na Ushirikiano wa Kimataifa, Bernard Membe, Dk. Emmanuel Nchimbi, Hussein Mwinyi na Waziri Mkuu Mstaafu, Frederick Sumaye na Waziri Mkuu wa sasa Mizengo Pinda.
Majina ya wanasiasa wengine wanaotajwa ni pamoja na Mathias Chikawe, John Magufuli, William Ngeleja, Lazaro Nyalandu na Ezekiel Maige.
Katika hatua nyingine, wakati Uchaguzi Mkuu wa Chama cha Mapinduzi (CCM), unatarajiwa kufanyika mwaka huu, chama hicho kimejikuta kikiingia kwenye vita mpya ya kinyang’anyiro cha kuwania nafasi ya Mwenyekiti wa Umoja wa Wazee na ile ya Umoja wa Vijana (UVCCM).
Ugumu wa uchaguzi huo, unatokana na makundi yanayowania urais ndani ya CCM mwaka 2015 kufanya kila iwezalo kuhakikisha inamwingiza mtu wake ambaye atapata nafasi ya kuingia kwenye vikao muhimu vya maamuzi, yaani Halmashauri Kuu (NEC) na Kamati Kuu (CC).
Tayari makundi hayo ya urais yameshaanza harakati za kuhakikisha yanashika nafasi hizo nyeti kwa gharama yoyote ile.
Kiti cha Mwenyekiti wa Wazazi CCM, kimeachwa wazi baada ya aliyekuwa kiongozi wa nafasi hiyo kufariki wiki iliyopita wakati nafasi ya umoja wa vijana iko wazi baada ya aliyekuwa Mwenyekiti wa Jumuiya hiyo, Masauni Masauni, kuamua kujiuzulu kutokana na kashfa ya kughushi umri wake.

URAIS 2015 CHADEMA,CCM HAPATOSHI ,,,,,,,,,,,,,,,KWA NINI??? ,,SOMA HAPA KUJUA SABABU


Katibu Mkuu wa chadema, Dk Willibroad 
Slaa
FUKUTO la Urais mwaka 2015 ndani ya vyama vya siasa linazidi kupamba moto, huku majina ya makada wanaowania nafasi hiyo kupitia chama kikuu cha upinzani nchini Chadema, yakianza kuanikwa.

Ikiwa imebaki takribani miaka mitatu kabla ya kufanyika Uchaguzi Mkuu wa Rais mwaka 2015, makada mbalimbali ndani ya vyama, wameanza kupigana vikumbo kila mmoja kujaribu kujipanga ili achaguliwe kupeperusha bendera ya chama chake kwenye uchaguzi huo. Ndani ya chama tawala CCM, taarifa zinadai kuwa baadhi ya wanasiasa wameanza kuunda mitandao huku wengine wakilaumiwa kuanza ‘kucheza rafu’ kwa kumwaga mamilioni ya fedha kwa lengo la kutekeleza mkakati huo.Tayari hatua hiyo imelaumiwa na baadhi ya makada ndani ya chama hicho kikongwe nchini huku wengine wakionya kuwa mbio za Urais mwaka 2015, zinatishia kuisambaratisha CCM.



Wakati heka heka hizo zikiendelea ndani ya CCM, habari kutoka ndani ya Chadema, zimetaja baadhi ya majina ya makada wa chama hicho, wanaopewa nafasi kubwa kugombea urais kwa tiketi ya chama hicho mwaka 2015.

Habari zilizopatikana kutoka ndani ya Chadema, zimewataja watu hao kuwa ni  Mwenyekiti wa chama hicho, Freeman Mbowe, Katibu Mkuu wa Chadema ambaye pia aligombea urais kupitia chama hicho kwenye uchaguzi uliopita, Dk Willibroad Slaa na Naibu Katibu Mkuu wa chama hicho, Zitto Kabwe.

Ingawa Zitto tayari ameweka wazi kuwa hatagombea kutokana na umri wake kuwa chini ya ule unaotambuliwa kikatiba kwa nafasi hiyo, bado ana matumaini kwamba kipengele hicho kinaweza kubadilishwa ndani ya katiba mpya.

Kwa mujibu wa katiba ya sasa, mtu anayewania Urais wa Jamhuri ya Muungano lazima awe na umri kuanzia miaka 40 na kuendelea. Mwaka 2015 Zitto atakuwa hajafikisha umri huo na ‘atanusurika’ endapo tu katiba mpya itapunguza umri huo.

Chanzo chetu kimeeleza kuwa picha halisi ya atakayewania nafasi ya urais kupitia chama hicho itadhihirika baada ya kukamilika kwa chaguzi za ngazi zote ndani ya chama hicho baadaye mwaka huu.

Mazingira mengine ambayo yanaweza kuathiri ama kuamua juu ya mgombea urais wa chama hichona kujiunga kwa wanachama wapya husasan kama baadhi ya vigogo watajiengua CCM na kuamua kujiunga na chama hicho.


Hofu ya makada wa CCM kutimkia Chadema inatokana na kundi kubwa la wanasiasa ndani ya chama hicho kutaka nafasi hiyo, hali itakayowafanya wengine kwenda vyama vingine kujaribu bahati zao.

Kutokana na idadi kubwa ya wanaCCM wanaotaka nafasi hiyo, baadhi ya watu wanadaiwa kuunda mitandao yenye malengo ya kuchafuana

CCM katika kikao chake cha Halmashuari Kuu (NEC) kilichoketi mjini Dodoma Novemba mwaka jana, kilikiri kuwa mvutano mkubwa wa makundi uliopo ndani ya chama hicho, chanzo chake ni Urais wa mwaka 2015.

Kwa upande wa Chadema, ingawa bado hakuna vita ya wazi wazi kama ilivyo ndani ya CCM, wanachama wake wameaanza kuzungumzia na kujipanga kwa ajili ya uchaguzi huo.

Dk Slaa ambaye aligombea katika uchaguzi uliopita na kuibuka mshindi wa pili baada ya kupata asilimia 26 ya kura zote zilizopigwa, ndiye anayeonekana kupewa nafasi kubwa. Mwanasiasa huyo anaonekana kuwa bado anafaa kuwania tena nafasi hiyo kutokana na rekodi nzuri kwenye uchaguzi uliopita.

Katika uchaguzi huo, Dk Slaa alionesha kuyaelewa vyema matatizo ya Watanzania na kujaribu kueleza nini kifanyike kuondokana nayo, hali iliyowafanya wananchi wengi kuwa na imani naye.

Mbowe (50) ambaye aliwania kiti cha urais mwaka 2005 na kushika nafasi ya tatu, anatajwa kuwa anaweza kuwania tena nafasi kutokana na rekodi yake safi ya kukiimarisha chama hicho kunzia tangu kikiwa kichanga hadi kukiwezesha kuwa chama kikuu cha upinzani nchini.


Wanachama wengine wa chama hicho wanaotajwa kuwania nafasi hiyo ni pamojan na John Shibuda ambaye mwaka juzi alichukua fomu za kuomba kuwania urais kupitia chama CCM, lakini baadaye alijitoa na kumuunga mkono mgombea wa chama hicho, Rais Kikwete.

Wengine ni Mbunge wa Singida Mashariki, Tundu Lissu, Mbunge wa Ubungo, John Mnyika, Mbunge wa Mbeya Mjini, Joseph Mbilinyi maarufu Sugu na Mbunge wa Nyamagana, Ezekiel Wenje na Mbunge wa Arusha Mjini, Godbless Lema.

Hata  hivyo Lema ambaye ametajwa kuwa mbunge bora kwenye moja ya mitandao ya kijamii nchini, aliliambia Mwananchi Jumapili juwa hana nia ya kuwania urais kupitia chama hicho mwaka 2015.

Alisema pamoja na kupata kura nyingi za watu waliomuunga mkono kwenye mtandao huo, alisema hatarajii kugombea nafasi hiyo ya urais ila akasisitiza kuwa ataweka nguvu zaidi kwenye ubunge."Nashukuru kwa kupata kura hizo, lakini sitarajii kuwania nafasi hiyo… Atakayeteuliwa na chama changu nitamuunga mkono," alisema.


Urais na migogoro
Imeelezwa kuwa migogoro mingi inayovikumba vyama vya siasa vikiwemo  NCCR -Mageuzi na CUF inachangiwa kwa kiasi kikubwa na mbio za Urais mwaka 2015.

Tayari NCCR- Mageuzi na imetangaza kumvua uanachama Mbunge wa Jimbo la Kigoma Kusini David Kafulila na wanachama wengine 11 huku CUF kikimfukuza Mbunge wa Wawi, Hamad Rashid Mohamed na wenzake, huku wanachama wengine wakipewa karipio kali.Hata hivyo, wabunge hao wamekataa kutambua kufukuzwa kwao huku wakifungua kesi Mahakama kuu kupinga  maamuzi vyama vyao.

Profesa Wangwe
Kuhusu nani anaweza kuteuliwa kugombea urais kupitia Chadema mwaka 2015, Mkurugenzi wa Taasisi ya Kuondoa Umasikini (Repoa), Profesa Samweli Wangwe alisema vyama vitakavyoteua wagombea ni lazima vichunguze kwa makini na kuona kwamba mgombea huyo  lazima awe na uwezo wa kuimarisha  uchumi ambao Watanzania wote wanaweza kushiriki katika kuujenga.

Alisema matatizo mengi ya kiuchumi yaliyopo nchini yanatokana na uchumi kusambaratika na wanaoshiriki katika kuujenga kuwa wachache."Mtu huyo lazima awe na mtazamo wa kiuchumi na ili mabadiliko hayo yawepo ni lazima ujengwe uchumi ambao watu wote pamoja na masikini wata-participate  (watashiriki).
Lakini akasema vyama vya upinzani hususan Chadema ambayo ilionekana kufanya vizuri katika uchaguzi uliopita, kitategemea kufanya vibaya kwa CCM ili kiweze kupata ushindi.
"Ili mgombea wa Chadema aweze kuchaguliwa itategemea sana kufanya vibaya kwa serikali ya CCM… Lakini ikifanya vizuri, itakuwa ni wakati mgumu kwao," alisema Profesa Wangwe.                                                     

Alipotakiwa kumtaja mtu ambaye anamuona kuwa anaweza kufanya vizuri kupitia Chadema, alisema ni vigumu kufanya hivyo kwa sababu hali hiyo inategemea sana ajenda ya chama hicho kwa mwaka 2015.

Alikiri kuwa Chadema kiliweza kuungwa mkono katika uchaguzi uliopita, lakini mipango yake kwa mwaka 2015 itategemea ajenda waliyo nayo na kufanya vibaya kwa serikali ya CCM.

Ndani ya CUF

Kwa upande wa CUF Mbunge wa Wawi aliyefukuzwa kutoka chama hicho hivi karibuni  Hamad Rashid amekataa kuuhusisha mgogoro huo na harakati zake za kutaka urais wa Zanzibar.

“Sikuyaanzisha mapambano haya kwa kutaka cheo. Mimi nilipewa uwaziri wakati wa Mwalimu Nyerere, lakini sikukubali, nikawaambia kuwa nitabaki tu na u-naibu Waziri wa Fedha” alisema Hamad na kuongeza;

“Mimi nimeshiriki kuanzisha CUF lakini sijawahi kuwa na uongozi mkubwa ndani ya chama, zaidi ya u-naibu Mkurugenzi tu. hata leo tukianzisha chama, wenzangu wakichagua viongozi, mimi niko radhi tu”.

Lakini kwa upande wake Naibu Katibu Mkuu wa chama hicho upande wa Zanzibar Ismail Jussa ametuhumu Hamad kufanya vurugu ndani ya CUF kwa lengo la kumpindua Maalim Seif katika nafasi ya ukatibu Mkuu, kisha kugombea urais.
 “Kama anapinga kutotaka cheo, basi Hamad anaanza kuchanganyikiwa. Mara ngapi katika matamshi yake amekuwa akitangaza kuitaka nafasi ya Ukatibu Mkuu. Anajidanganya,” alisema Jussa na kuongeza,

“Kikwete Ameliingiza Taifa Vitani”….Dk. Slaa

SLAA
KAULI aliyopata kuitoa Waziri Mkuu Mizengo Pinda bungeni kuwataka polisi wawapige wapinzani, na kauli ya juzi ya Rais Jakaya Kikwete kuwaagiza wafuasi wa Chama Cha Mapinduzi (CCM), wajibu mapigo pale wanaposhambuliwa na wapinzani, imeelezwa kuliingia taifa vitani.
Akifungua kikao cha Halmashauri Kuu (NEC) ya CCM taifa mjini Dodoma, Rais Kikwete ambaye ni mwenyekiti wa chama hicho taifa, alisema bila kumung’unya maneno akiwataka Wana-CCM kuacha unyonge na kujibu mashambulizi pale wapinzani wanapoendesha siasa za vurugu.
Waziri Mkuu Pinda katika kipindi cha Maswali na Majibu bungeni aliwahi kutoa kauli ya kuwataka polisi wawapige wafuasi wa CHADEMA kwa vile walikuwa wakiendesha maandamano katika sehemu mbalimbali nchini, ambayo Serikali ya CCM ilitafsiri kama vurugu.
Pinda ambaye hivi sasa amefunguliwa kesi mahakamani ya kuvunja katiba kutokana na kauli hiyo, alisema serikali imechoka na haina njia nyingine zaidi ya kuwataka polisi wawapige wapinzani.
Wakitoa maoni yao kuhusu msimamo wa Rais Kikwete, baadhi ya wanazuoni, viongozi wa siasa wameeleza kushangazwa na kauli ya kiongozi huyo mkuu wa nchi kwani ameliingiza taifa vitani.
Katibu Mkuu wa Chama cha Demokrasia na Maendeleo (CHADEMA), Dk. Willibrod Slaa, amesema kauli ya Rais Kikwete inatisha, inashangaza na haikupaswa kutolewa na kiongozi mkuu wa nchi.
Alisema kauli yoyote inayotolewa na rais pasipo kujali yupo sehemu gani ni amri kwa walio chini yake, na kwamba kinachofuata ni utekelezaji.
“Waswahili wanasema ukishangaa ya Musa utaona ya Firauni. Hivi karibuni tulishangaa kauli ya Pinda kutaka polisi wawapige tu wapinzani, leo rais naye anawataka CCM waache unyonge, wajibu mapigo. Hii ni hatari sana,” alisema Dk. Slaa.
“Kwa maoni yetu, CHADEMA tunasema Rais Kikwete ameliingiza taifa vitani, amefungua milango ya uvunjifu wa amani, kinachofuata ni umwagaji damu.”
Dk. Slaa aliongeza kwa kusema kuwa anatilia shaka uwezo wa Rais Kikwete katika kuchambua taarifa
anazofikishiwa mezani na wasaidizi wake, ambazo safari hii zimemfanya aamini wanaoanzisha vurugu katika uchaguzi ni wapinzani.
Alisema licha ya Tume ya Jaji Amir Manento na ile ya Haki za Binadamu kulitaja Jeshi la Polisi na CCM kuwa chanzo cha vurugu zinazosababisha mauaji ya watu nchini, Rais Kikwete ameziba masikio na kuwarushia tuhuma hizo wapinzani.
“Watu wameuawa Nyololo na Arusha, ripoti ya Haki za Binadamu anayo ofisini kwake ameifungia na kisha ametoa zawadi ya kuwapandisha vyeo wale waliosababisha mauaji hayo, leo anathubutu vipi kusema wapinzani ndio chanzo cha vurugu?” alisema na kuhoji Dk. Slaa.
Alisisitiza kuwa licha ya Rais Kikwete kuwasingizia wapinzani kuwa chanzo cha fujo, bado ameshindwa kuunda tume huru ya kimahakama ili kuujua ukweli wa matukio hayo.
Alisema kimsingi CHADEMA haitakubali damu ya Mtanzania hata mmoja imwagike kwa sababu ya kupata madaraka, na kwamba agizo la Rais Kikwete linavilazimisha vyama vya upinzani kuwaandaa vijana wao ili kujilinda.
“Hivi kama na sisi tutaamua kuwaambia vijana wetu wajilinde, na katika hali hii ya kunyanyaswa na kuonewa na hao CCM kwa kushirikiana na vyombo vya dola, unadhani nchi itabaki salama?” alihoji Dk Slaa.
Mwenyekiti wa Chama Wananchi (CUF), Profesa Ibrahim Lipumba, amemsikitikia Rais Kikwete kwa kupoteza uelekeo wa kulinda amani ya nchi.
Alisema ameshtushwa na kauli hiyo aliyoieleza kuwa imekosa uvumilivu wa kisiasa, huku akiainisha kuwa chanzo cha vurugu katika sehemu mbalimbali nchini ni CCM kwa kushirikiana na vyombo vya dola.
Alisema alitegemea Rais Kikwete ahimize Watanzania kutii sheria bila shuruti badala ya kuonyesha dalili za wazi kuwa hakuna haja ya kutii sheria, na hata vyombo vinavyotafsiri sheria hiyo.
“CCM ndio waanzilishi wa vurugu zote nchini, na kama mwenyekiti wao ametoa kauli hiyo, unategemea nini kitatokea ikiwa yeye ndiye amiri jeshi mkuu?” alihoji Lipumba.
Mwenyekiti wa NCCR-Mageuzi, James Mbatia, kwa upande wake alisema kauli ya Rais Kikwete itamfanya abebe dhamana juu ya jambo lolote la uvunjifu wa amani litakalotokea kuanzia sasa.
Alisema ni hivi karibuni taifa liliingia katika maridhiano ya kuandika katiba mpya kwa ajili ya Watanzania, hivyo Rais Kikwete hakupaswa kutoa kauli hiyo wakati huu.
“Hii kauli haina viashiria vizuri kwa taifa, ni vema aje hadharani atuambie alikusudia nini, vinginevyo atabeba dhamana ya jambo lolote litakalojitokeza,” alisema.
Mhadhiri mwandamizi wa Chuo Kikuu cha Dar es Salaam (UDSM), ambaye ni mchambuzi wa masuala ya kisiasa na jamii, Bashiru Ally, alisema Watanzania wategemee visa vingi wakati huu wa kuelekea uchaguzi wa 2015.
Alisema nchi inaweza kuingia kwenye machafuko ambayo hayajawahi kutokea
kutokana na kauli za wanasiasa, zinazolenga kuwanufaisha wao binafsi badala ya maslahi ya taifa.
Aliongeza kuwa kitendo cha Mwenyekiti wa CCM kuwaagiza wafuasi wake wasiwe wanyonge na wajibu mapigo, siyo suluhisho la tatizo bali ni kuongeza tatizo.
Alisema NEC ya CCM badala ya kukaa na kuamua kupambana, wangetafuta jibu juu ya kiini cha mapambano hayo yanayodaiwa kutokea katika jamii.
“Mwenyekiti amekuja na majibu mepesi katika maswali magumu, na mimi nasema kuchoka uvumilivu si jawabu la tatizo, wajitokeze hadharani kutibu chanzo,” alisema Bashiru.
Alisema rais kuruhusu hali hiyo ni kutangaza vita ya wenyewe kwa
wenyewe kwa kuwa kauli yake ni amri kwa walio chini yake, na kwamba wananchi watakapokataa kunyanyaswa, madhara yake yatakuwa makubwa kwa jamii nzima.
Mkuu wa Jeshi la Polisi nchini (IGP), Ernest Mangu, alipoulizwa kama kauli ya rais inaashiria Jeshi la Polisi limeshindwa kutekeleza wajibu wake wa kuwalinda Watanzania na pia kama si uchochezi wa wazi, alisema hajapata taarifa hizo wala kusikia, na kwamba atafanyia kazi ajue kama alichoelezwa kimetamkwa na Mwenyekiti wa CCM Taifa.
“Mimi ndiyo kwanza ninasikia kutoka kwako, wewe ndiyo unaniambia, ngoja nifuatilie nijue kama kauli hiyo imetolewa na Mwenyekiti wa CCM,” alisema IGP Mangu.
Akifungua mkutano wa NEC ya CCM juzi mjini Dodoma, Rais Kikwete aliwataka wanachama wa chama hicho kuacha unyonge kwani uvumilivu waliokuwa nao umefika kikomo chake.
SLAA
Alisema chama hicho kinaingia kwenye uchaguzi mdogo katika Jimbo la Kalenga mkoani Iringa, kinashindana na vyama vingine ambavyo alisema ni wagomvi, maana kwao ugomvi ndiyo sehemu ya mwongozo wa kufanya kazi ya siasa.
“Tulizungumza nalo hilo kwenye Kamati Kuu, tulikubaliana kuacha unyonge. Ndiyo, kwenye Kamati Kuu tumekubaliana, tumesema jamani watu wote waende wakaseme tumekubaliana kuacha unyonge,” alisema huku akicheka na kupigiwa makofi na wajumbe wa NEC.
Rais Kikwete ambaye pia ni Amiri Jeshi Mkuu, alitolea mfano wa tukio lilitokea Kahama mkoani Shinyanga, ambapo kijana mmoja alitolewa macho kwa bisibisi, na tukio la Igunga ambapo kijana mmoja alimwagiwa tindikali katika uchaguzi mdogo wa jimbo hilo.
“Acheni unyonge na hata katika taarifa ya habari leo (jana) mtoe hivyo hivyo. Na muache habari zote mseme hii tu (waandishi wa habari). Uvumilivu una ukomo wake,” alisema huku wajumbe wakiendelea kumpigia makofi.
“Nalisema kwa sababu yanayotokea yanasikitisha sana. Pale Igunga kijana yule wamemmwagia tindikali, pale Kahama kijana ametolewa macho kwa bisibisi,” alisema.
Uchaguzi mdogo wa ubunge Jimbo la Kalenga lililopo mkoani Iringa unatarajiwa kufanyika Machi 16, mwaka huu, huku tayari vyama vya CCM na CHADEMA vikiwa vimetaja wagombea wao.