Tuesday, 18 February 2014

Juma Nature Akana Madai ya Kumponda Diamond kwenye Nyimbo yake Mpya…Adai ‘Dada Mondi’ ni Msanii tofauti.

nature
Hatimaye Juma Nature, amezungumzia utata ulioibuka kwenye wimbo wake mpya Kama Jana, unaohusiana na kama kweli amemdiss Diamond.
Akiongea na kipindi cha Showtime Next Chapter, Juma Nature aka Kiroboto amesema jina la ‘Dada Mondi’ lililofanya wengi waamini kuwa ni version yake ya Diamond, ni jina la msanii mwingine kabisa.
“Hamna diss ya kumdiss Diamond, Diamond hajadisiwa,” amesema Nature.
“Pale katajwa mtu mwingine kabisa anaitwa Dada Mondi na anakaa mitaa ya kwetu. Bado hajatoka halafu anataka sifa.”
nature

0 comments:

Post a Comment