MSANII wa filamu Elizabeth Michael Kimemeta (18), maarufu kama Lulu anayekabiliwa na kesi ya mauaji ya bila kukusudia ya msanii mwenzake Steven Kanumba (28), leo amekiri mahakamani kwamba siku ya tukio alikuwa na ugomvi na marehemu kabla ya kifo chake.
Kadhalika,
alikiri kuwa walikuwa na uhusiano wa kimapenzi na kwamba alikuwa na
utamaduni wa kumtembelea marehemu Kanumba nyumbani kwake Sinza, jijini
Dar es Salaam.
Lulu
alitoa madai hayo leo wakati akisomewa maelezo ya awali baada ya
kusomewa mashtaka yake mbele ya Jaji Rose Teemba aliyepangiwa kusikiliza
kesi hiyo. Upande wa Jamhuri uliongozwa na Wakili wa Serikali Mwandamizi Monika Mbogo, Wakili wa utetezi Peter Kibatala.
Saa 6:00 mchana Lulu alipanda kizimbani na kusomewa mashtaka yake kwamba Aprili 7, mwaka jana Sinza Vatican, jijini Dar es Salaam, mshtakiwa alimuua Kanumba bila kukusudia na alikana mashitaka yake. Mbogo alimsomea mshtakiwa maelezo yake kwamba Lulu alikuwa na kawaida ya kumtembelea Kanumba nyumbani kwake na kwamba walikuwa na uhusiano wa kimapenzi.
Upande wa Jamhuri ulidai kuwa, Kanumba wakati wa uhai wake alikuwa akiishi na mdogo wake Seth Bosco na siku ya tukio alimtaka mdogo wake huyo ajiandae watoke kwenda kwenye starehe saa 6:00 usiku.
Wakili huyo aliendelea kudai kuwa siku ya tukio Lulu alikwenda nyumbani kwa Kanumba saa 6:00 na alipitiliza hadi chumbani. Ilidaiwa
kuwa Seth alisikia Lulu na Kanumba wakilumbana na alimsikia marehemu
Kanumba akihoji ‘kwa nini unaongea na bwana wake mbele yake’ alinukuliwa
marehemu.
Ilidaiwa
kuwa Seth alisogelea mlango akamuona Lulu anahangaika kutafuta upenyo
wa kutokea chumbani na kwamba alimuona kaka yake akimvuta na kufunga
mlango wa chumba kwa ndani.
Alidai kuwa Seth alimuona mshtakiwa akitoka chumbani kwa marehemu na kumweleza kwamba kaka yake ameanguka. Ilidaiwa kuwa Seth alimpigia simu daktari binafsi wa Kanumba na baada ya kumfanyia uchunguzi aligundua amekufa lakini aliwaagiza wampeleke Hospitali ya Taifa Muhimbili alikotangazwa kifo chake.
Alidai kuwa Seth alimuona mshtakiwa akitoka chumbani kwa marehemu na kumweleza kwamba kaka yake ameanguka. Ilidaiwa kuwa Seth alimpigia simu daktari binafsi wa Kanumba na baada ya kumfanyia uchunguzi aligundua amekufa lakini aliwaagiza wampeleke Hospitali ya Taifa Muhimbili alikotangazwa kifo chake.
Mbogo alidai kuwa upande wa Jamhuri unatarajia kuwasilisha vielelezo viwili vya maelezo ya onyo ya mshitakiwa na ripoti ya kifo cha marehemu Kanumba. Katika ripoti ya daktari inaonyesha kwamba kifo cha Kanumba kilitokana na kushindwa kupumua kutokana na mtikisiko uliosababisha ubongo kuvimba.
Jaji Teemba alisema baada ya maelezo hayo dhamana ya mshtakiwa inaendelea na kesi itasikilizwa tarehe itakayopangwa na mahakama na pande zote mbili zitajulishwa.
0 comments:
Post a Comment