Tuesday, 18 February 2014

Serikali ya Syria yaingia lawamani


Wajumbe katika mkutano wa amani wa Geneva.
Mataifa ya Ufaransa na Uingereza yameilaumu Serikali ya Syria kwa kuanguka kwa mazungumzo kati yake na upinzani mjini Geneva.
waziri wa maswala ya kigeni nchini Ufaransa amesema kuwa wajumbe wa rais Assad walipinga mipango yote ya kubuni serikali ya mpito.
Mpatanishi mkuu wa umoja wa mataifa Lakhdar Brahimi aliomba msamaha kwa raia wa Syria kwa tukio hilo.
Amesema alishindwa kubuni tarehe nyengine ya mazungumzo,huku akitoa matumaini kwamba vikao hivyo vitalazimika kuendelea katika siku za usoni.
Wanaharakati wanasema kuwa takriban raia elfu sita wa Syria wameuawa tangia awamu ya kwanza ya mazungumzo hayo ianze mwezi uliopita.

0 comments:

Post a Comment