KUNA
mambo ambayo yanaweza kuonekana ya kawaida tu au si ya lazima sana
lakini kumbe yana uzito na thamani kubwa sana kwenye uhusiano. Wengi
wakitaka kufanya jambo la kumfurahisha mpenzi wake, huwaza katika
ukubwa.Wapo wanaofikiri labda kwa kutoka na mwezi wake kwenda naye
kwenye hoteli kubwa ya kifahari ya nyota tano na kulala kwa usiku mmoja
lina thamani kubwa. Pengine wapo wanaofikiri kuwa, kuwanunulia wenzi wao
vitu vya thamani kubwa kama cheni ya dhahabu, gari n.k ndivyo vyenye
thamani pekee!
Si
kweli. Ni ukweli usio na shaka kwamba, mwanamke anapenda kufanyiwa vitu
vyenye thamani na mwanaume wake. Ukweli unabaki kuwa, wakati mwingine
unaweza kuwa unatamani kumfanya mwenzi wako awe na furaha muda wote
lakini mfuko wako ukawa hauruhusu!
USISAHAU KUUNGANA NASI KWA KULIKE PAGE YETU HAPA
Hulka
ya wanawake wengi ni kutamani kuona mwenzi wake anamuona ni mtu muhimu
na anakuwa naye karibu muda wote. Wanawake hawajali sana vitu vya
thamani kama wanaume wanavyofikiri.
Kumkumbatia
mwanamke na kumbusu katikati ya midomo yake, ukisindikiza na maneno
matamu ni zaidi ya gari utakalomnunulia – kikubwa hapa, mwanamke huyo
awe kweli ana upendo nawe na si kuwa yupo kibiashara!
Katika mada hii, nimekuandalia vitu vichache ambavyo kwa hakika, kwa mujibu wa utafiti nilioufanya, ni ‘sumu’ kwa wanawake.
Ukifanya vyote au sehemu yake, unamfanya mwanamke wako ajihisi yupo katika mikono salama.
Bado
thamani ya mali na vitu vingine vitabaki katika uhalisia wake, lakini
kwa hakika mambo yafuatayo hapa chini, huwachanganya sana wanawake.
KADI
Ni
utaratibu uliozoeleka sana kipindi cha nyuma kidogo. Sasa hivi
teknolojia imeongezeka, kadi inaweza kupatikana hata kwenye mitandao
mbalimbali ya internet. Hata hivyo, bado inaonekana kuwa mwanamke
anapenda na anatamani kuona mwanaume wake anamkumbuka kwa kumtumia
kadi.
Wanaume
wengi ni wavivu, lakini kwa sababu ya ustawi wa penzi lako, jaribu
hili. Nunua kadi yako yenye ujumbe mzuri, andika maneno mengine kwa
mkono wako mwenyewe, pulizia manukato unayotumia, kisha mtumie/ mpelekee
mpenzi wako. Utakuwa umemroga!
NYIMBO, MASHAIRI
Wanawake
wanapenda sana kufahamu kuwa kweli alipo anapendwa. Nyimbo nzuri za
mapenzi ambazo zitaeleza uzuri wake na namna unavyompenda na kumthamini,
vinazidi kukuweka katika kilele cha umiliki uliotukuka.
Mchagulie
mpenzi wako wimbo redioni, taja jina lake, lako na ujumbe wako.
Utamfanya ajisikie fahari sana. Mashairi katika magazeti mbalimbali na
majarida pia huongeza ladha ya mapenzi.Anachojali
mwanamke ni ile hali ya kuona kuwa, unampenda na unaweza kuthibitisha
hilo hata mbele ya watu wengine. Kusikia akitajwa redioni au ameandikwa
gazetini ukionyesha hisia zako za kumpenda, kutamchanganya na kumfunga
kabisa hisia za kufikiri kukusaliti.
Tatizo wanaume wengi hawatilii maanani haya mambo lakini kama unataka kuwa dume la mbegu kwa mwanamke wako, jaribu uchawi huu.
0 comments:
Post a Comment