Showing posts with label tukio. Show all posts
Showing posts with label tukio. Show all posts

Wednesday, 19 February 2014

HABARI ZA IVI PUNDE..!! MAPIGANO BAINA YA WAHUNI NA WAENDESHA BODABODA YAENDELEA HUKO MBEZU JUU DAR ES SALAAM

 Hili ni kundi la vijana waendesha bodaboda wakienda mtoni kumwokoa mwenzao ambaye wanadai ametekwa na wahuni wanaojificha mtoni na kukaba watu, mpaka sasa boda boda aliyetekwa yupo mwananyamala hospital na mmoja wa vijana wanaoaaminika kwamba ni vibakaba ameshauawa
Kuna mapigano makali eneo la kwa mzee Juma Kata ya Mbezi juu.
Habari zaidi zionasema kwamba Waendesha Bodaboda hao wanaendelea kupambana kwa kutumia silaha za jadi dhidi ya vijana wanaosemekana aidha 
ni vibaka au wameiba pikipiki ya mwenzao.
Hali ni mbaya majeruhi ni wengi na inasemekana kuna vifo vimetokea.

Tuesday, 18 February 2014

. HABARI MPYA !!!! RUBANI MSAIDI ATEKA NDEGE YA SHIRIKA LA NDEGE LA ETHIOPIAN AIRLINES.

Ndege iliyokuwa imetekwa

Rubani msaidizi wa ndege ya abiria ya shirika la ndege la Ethiopia ndiye aliyeiteka nyara.
Maafisa mini Geneva wanasema kuwa naibu huyo wa rubani alichukua usukani wa ndege hiyo rubani wake alipokwenda msalani kwa haja.


Tukio hilo inaripotiwa kutokea ndege hiyo aina ya

Boeing 767-300 ilipokuwa ikipaa katika anga ya Sudan.
Rubani huyo msaidizi alibadili mkondo wa ndege hiyo iliyokuwa ikielekea Rome Italia ,na kuipaa hadi Uswisi alipoitua katika uwanja wa ndege wa Geneva.



Katika taarifa kwa vyombo vya habari shirika hilo linasema kuwa abiria wote 200 wako salama .
Ripoti ya idara inayosimamia usafiri wa ndege ya Uswisi inasema kuwa rubani huyo msaidizi aliomba uraiya kabla ya kutua ndege hiyo na akajisalimisha kwa maafisa wa usalama waliokuwa wameizingira ndege hiyo.
Polisi walimtia mbaroni mara moja .Chanzo BBC Swahili



The path of the plane circling over Geneva, captured by flightradar24.com.

Monday, 17 February 2014

HIII,,,,,,,,,NOMAAAAAAAAAAA,,,,MCHAWI AJIKUTA APATA AJALI NA UNGO WAKE,,,,,,SOMA KUJUA,,,,,


 
HALI ya taharuki iliyoambatana na imani za kishirikina iligubika Jiji  la  Arusha kufuatia mwanamke ambaye hakufahamika jina kudondoka na ungo wa kishirikina asubuhi ya Ijumaa iliyopita kisha ghafla kubadilika  kuwa kuku mweupe mwenye mayai ndani ya ungo, Uwazi limeona mengi.
Mamia ya wananchi katika eneo la Kimandolu kando ya Barabara ya Arusha- Moshi walimiminika kushuhudia tukio hilo lililojiri saa tatu asubuhi.
Akizungumza na Uwazi, shuhuda mmoja wa tukio hilo ambaye ni dereva wa bodaboda, Martin Mbise alisema:
“Nilikuwa kwenye shughuli zangu za kila siku, ghafla niliona kitu kipana kikidondokea kwenye huu mtaro, ndani yake nikamwona mtu amekaa akiwa uchi wa mnyama.

“Wengi tuliamua kusogelea eneo la tukio, lakini kabla hatujakifika, mtu huyo alitoweka, badala yake mle mwenye ungo  mkawa na kuku mweupe na mayai zaidi ya kumi, tulishangaa sana:
Mbise alisema hali hiyo ilidumi kwa saa mbili na nusu, ndipo wananchi hao wakaamua kumchoma moto kuku huyo baada ya kumuua na kuyavunja mayai.

Hata hivyo, alisema haikuwa rahisi kuku huyo kuungua licha ya kumwagiwa mafuta ya taa na petroli na wakachukua uamuzi wa kumkatakata na kugawana nyama yake huku baadhi
yao wakikimbia hovyo na kulaani tukio hilo.

Baadhi ya wakazi wa eneo hilo walisema tukio hilo ni laana na anapaswa kuitwa mtumishi wa Mungu kwa ajili ya kukemea pepo mchafu kwa maombi ya kiroho wakiamini mchawi huyo alikuwa ana lengo la kuwadhuru.
Kamanda wa Polisi Mkoa wa Arusha, ACP Lebaratus Sabas hakuweza kupatikana kuzungumzia tukio hilo, lakini baadhi ya maafande waliofika katika eneo hilo walithibitisha.

Sunday, 16 February 2014

MAAJABU YA DUNIA,,,: HANDAKI LA AJABU LAONEKANA ENEO LA KITANZINI IRINGA.. SHUHUDIA



 Umati wa watu waliofika katika eneo la kitanzini kuangalia handaki hilo
 mkuu wa Wilaya Ya Iringa mjioni Dkt Leticia Warioba akihojiana na mmiliki wa numba ambayo handaki hilo limeonekana
 Handaki lenyewe muonekano wa sehemu ya kuingilia
 Mkuu wa Wilaya kushoto aipokea maelekezo kutoka kwa mmoja wa wafanyakazio wa kampuni ya maji Iringa

 Wananchi wakendelea kutazama kila mmoja akiwaza lake

Handaki la ajabu limeonekana katika eneo la kata ya kitanzini mtaa wa sokoni
Katika tukio hilo lililokuwa gumzo kubwa katika eneo hilo huku kila mmoja akisema lake
Mtandao huu ulipokutana na mmiliki wa nyumba hiyo hakuweza kuwa na majibu yakuridhisha  huku akisema yeye hafahamu shimo hilo limetokea wapi.

Handaki hilo ambalo lilionekana jana na wachimbaji wa mitaro wa JR wanaoshuhulika na  uwekwaji wa mabomba mapya ya maji safi wanaeleza katika kuchimba ndipo walipokutana na chemba hiyo ikiwa imefunikwa na kudhani kuwa inatumika kama shimo la choo ya nje lakini haikuwa hivyo maana lilikuwa wazi limejengewa na hakuna dalili ya kutumika kama choo.

Akizungumza mmoja wa wananchi aliyeingia katika handaki hilo Abdukareem ameeleza kuwa yeye ni mkazi wa eneo hilo na alipopata taarifa alifika akiwa na mwenzake aliyefahamika kwa jina la Salehe na kukubaliana kuingia ndani ili kufahamu kilichopo.

Ameeleza kutokana na shimo hilo kuwa refu walitafuta ngazi lakini hawakufanikiwa kwani ngazi hiyo ilikuwa pana na kuamua kutafuta fimbo kubwa ya muanzi na kamba na ndipo walipofanikiwa kuingia ndani.

Anazidi kueleza kuwa walipofika ndani walikuta chumba ambacho ni kama futi tatu na kuona vidirisha vidogo kwa mbele huku bado kukiwa kumejengewa kwa zege na kubainisha kuna muendelezo wa chemba nyingine ambapo hawakuweza kuendelea kutokana na kuzibwa.

mkuu wa Wilaya afika eneo la tukio

Mkuu wa wilaya ya Iringa Dkt Leticia Warioba akafika katika eneo la tukio huku akiwa na wa wafanyakazi wa  Kampuni ya JR pamoja na afisa wa usalama ambao waliishia kuangalia njia hiyo pasipo kuingia ndani ya handaki hilo.

nini maoni ya wakazi waliofika katika eneo hilo?

Wengi wa wakazi waliofika katika eneo hilo hawakusita kueleza hisia zao huku wengine wakieleza labda ni mahandaki yaliyokuwa yakitumiwa na Wajerumani enzi za ukoloni, huku wengine wakieleza labda handaki hilo limekuwa likitumiwa na majambazi kama sehemu za kujificha na kuhifadhia mali walizoiba japo hapakuonekana na mali aina yeyote.

Kaliiiiiiiii y Mwaka,,,,,,,,,,,Mgonjwa wa akili atoa kali ya mwaka hospitalini



MKAZI wa Korogwe, mkoani Tanga ambaye inadaiwa alilazwa katika Hospitali ya Wagonjwa wa Akili Lutindi, wilayani humo,
hivi karibuni alitoa kali ya mwaka baada ya kutoka wodini, kuingia katika gari ambalo dereva wake alikuwa hajalizima na kuondoka nalo akiendesha mwenyewe.


Tukio hilo lilivuta hisia za watu wengi waishio jirani na hospitali hiyo, ambapo dereva wa gari hilo alifahamika kwa jina moja la Bw. Wikama ambaye aliliacha gari hilo likiwa halijazimwa.

Akizungumza na gazeti hili, Diwani wa Viti Maalumu Tarafa ya Bungu, Bi. Elizabeth Singano, alisema mgonjwa huyo wa akili ambaye jina lake halikuweza kupatikana mara moja, aliendesha
gari hilo na kushuka nalo katika milima yenye miteremko mikali
yenye kona bila wasiwasi wowote.

“Ilibidi zipigwe simu ili kuomba msaaada wa kulizuia gari ndipo wananchi waliamua kuweka magogo barabarani ili kulizuia,” alisema Bi. Singano anayekaa kitongoji cha Bethelehemu
kilichopo jirani na hospitali hiyo.

Aliongeza kuwa, Bw. Wikama alifika katika kituo hicho baada ya kupeleka mgonjwa wa akili na alipoteremka kwenye gari hakulizima ndipo mgonjwa huyo aliingia na kulichukua.

“Watu walishtuka walipoona mgonjwa wa akili akiendesha gari, walianza kupiga kelele wakati akiondoka nalo lakini mwenyewe hakuonesha waziwasi wowote,” alisema.

Majira lilipomtafuta Bw. Wikama ambaye ni mkazi wa Donge, jijini humo kwa njia ya simu ili kuzungumzia mkasa huo, alikiri kutokea tukio hilo na kudai kuwa, asingependa kulizungumzia kwa kina kwani gari hilo ni mali ya ofisi si la kwake.

“Ni kweli bwana mgonjwa wa akili aliendesha gari nililokwenda nalo hospitali ila nisingependa kulizungumzia sana tukio hilo, wapo watakaolipokea tofautina,” alisema Bw. Wikama ambaye alipotakiwa kutaja namba za gari na aina yake alikata simu
na alipopigiwa tena hakupokea.

Hata hivyo, Ofisa Utawala wa hospitali hiyo aliyefahamika kwa jina moja na Bw. Lauth, alipoulizwa kuhusu tukio hilo alikiri kutokea kwa tukio hilo na kudai mgonjwa huyo wamemrudisha Dar es Salaam.

Alisema tukio hilo halikuwa la kawaida lakini limetokea kwa sababu aliyefika na gari hospitalini hapo hakulizima kama ilivyo kawaida ya madereva wanaopeleka wagonjwa ili kuepuka matukio ya aina hiyo.