Mkazi mmoja wa Nzega, mkoani
Tabora, Juma Kiyabo (45) amemchija mke wake, Wande Monera (34), kabla ya
mwenyewe kunusurika kifo baada ya kujijeruhi vibaya shingoni katika jaribio la
kutaka kujiua.
Tukio hilo limetokea katika kijiji cha Tazengwa saa 7 usiku wa Februari 16
mwaka huu, huku ikielezwa kuwa sababu ya tukio hilo ni kunyimana unyumba mara
kwa mara.
Kaimu Kamanda wa Polisi, ambaye pia ni Mratibu Msaidizi mkoani Tabora, John Kauga amethibitisha kutokea kwa tukio hilo.
Kaunga alisema taarifa za awali zinaonyesha kuwa, mtuhumiwa alikuwa akigombana na mkewe mara kwa mara kwa sababu ya kunyimwa unyumba kabla ya kuamua kuchukua hatua hiyo mbaya.
Kamanda Kaunga alisema kuwa, mtuhumiwa baada ya kufanya unyama huo, naye alijikata koo kwa lengo la kujiua, lakini hata hivyo jaribio lake lilishindikana na sasa yuko chini ya ulinzi wa polisi.
0 comments:
Post a Comment