Wednesday, 6 November 2013

PICHA ZINATISHA ...AJALI MBAYA YA PIKIPIKI YAUA HUKO MWANZA


Watu wawili wamefariki dunia papo hapo wilayani Bukombe mkoani Geita wakitumia usafiri wa bodaboda kufuatia pikipiki waliyokuwa wakisafiria kuteleza kwenye mchanga ikiwa kwenye mwendo kasi na kisha kukanyagwa vibaya vichwani na gari aina ya Noah ambayo walikuwa wakipishana nayo.

 
Kwa mujibu wa shuhuda wa tukio hilo,  dereva wa bodaboda ambaye alikuwa na abiria wake mwanamke mwenye mizigo, alikuwa katika mwendo wa kasi. 

Hatua kadhaa kabla ya kupishana na gari hilo, matairi ya pikipiki yake yalishindwa kuhimili mchanga uliopo barabarani ndipo alipokosa uwiano wa kumiliki chombo hicho cha usafiri na kutereza kisha wakaanguka katikati ya barabara.
 
Sekunde chache gari la abiria aina ya Noah ambalo mpaka shuhuda huyo anaondoka kwenye tukio la ajali hakufanikiwa kulinasa namba zake likiwa kwenye kasi liliwapitia vichwani bodaboda na abiria wake ambao walikufa papo hapo.
 

0 comments:

Post a Comment