Misaada ya hali na mali imeanza kumiminika kwa
ajili ya Aida Nakawala (25) mkaazi wa kijiji cha Chiwanda, Wilaya ya
Momba, Mkoa wa Mbeya, ambaye alijifungua watoto wanne mapacha kwa mkupuo
(Quadruplets) usiku wa kuamkia Mwaka mpya wa 2014 katika Hospitali ya
Wazazi ya META jijini Mbeya.
Msamaria mwema wa Uingereza, Bi Gladness Sariah,
ametuma maboksi mawili yenye nguo na vitu kadhaa vya watoto, ambavyo
vimewasili salama katika ofisi za Michuzi Media Group (MMG) inayoendesha
Globu ya Jamii jijini Dar es salaam baada ya kusafirishwa bure na Wazee
wa Kazi, Serengeti Freight Forwarders ya huko Uingereza.
Hivi sasa MMG ikishirikiana na waratibu wa misaada kwa
mama huyo, Mbeya Yetu Blog, wanaandaa utaratibu wa kumfikishia Mama
Aida mizigo yake haraka iwezekanavyo.
Kwa niaba ya mzazi wa mapacha hao, Michuzi Blog na
Mbeya Blog zinatoa shukrani za dhati kwa msamaria mwema Gladness Sariah
kwa wema na upendo aliouelekeza kwa mzazi huyo. Huo ni mfano wa kuigwa,
na tunatarajia misaada zaidi itatolewa na wasamaria wema ambao tunajua
mko wengi kila kona ya dunia.
Kama umeguswa na hili na unataka kutoa msaada
tafadhali wasiliana na issamichuzi@gmail.com ama j.mwaisango@tonemg.com
nasi tutafikisha ubani wako.
Aida Nakawala 25 mkazi wa kijiji cha Chiwanda
Wilaya ya Momba Mkoa wa Mbeya, hivi karibuni alijifungua watoto wanne
mapacha kwa mkupuo(Quadliplets) katika usiku wa kuamkia Mwaka mpya
anaendelea vizuri.
Mwanamke huyo ambaye kwa hivi sasa anaendelea na
matibabu katika Hospitali ya Wazazi ya Meta akiwa na watoto wake wote
wanne alijifungua majira ya saa 10 alfajiri usiku wa kuamkia Januari
Mosi Mwaka huu katika Hospitali ya Wilaya ya Mbozi na watoto wakiwa na
uzito wa kawaida tofauti na matarajio ya Wengi.
0 comments:
Post a Comment