WANAFUNZI wa chuo cha ualimu Kleruu kilichopo
Gangilonga mjini Iringa, wamefanya maandamano wakipinga kukosa huduma ya
umeme kwa wiki ya tatu sasa baada ya Shirika la Umeme Tanzania
(Tanesco) kuwakatia.
Maandamano hayo yaliyoanzia chuoni hapo leo kuelekea
ofisini na hatimaye nyumbani kwa Mkuu wa Mkoa wa Iringa, yalidhibitiwa
na Jeshi la Polisi yakiwa yamekaribi shule ya msingi Um-salam kwa kile
kilichoelezwa kwamba hayakuwa na kibali..
Rais wa serikali ya wanafunzi ya chuo hicho, Manfred
Joachim alisema wametii amri ya Polisi lakini watayafanya tena Jumatatu
baada ya kukamilisha taratibu zote ikiwa ni pamoja na kupata kibali cha
Polisi.
Joachim alisema wameamua kutumia mbinu hiyo ili kuongeza msukomo kwa uongozi wa chuo na serikali kuitatua kero hiyo.
“Hatuwezi tena kujisomea usiku na mafunzo ya teknlojia
ya habari na mawasiliani yaani ICT yamesimama; wanafunzi wamekata tamaa,
hawajui hatma yao wakati ada wamelipa,” alisema.
Wakiwa wamekusanyika katika uwanja wa michezo wa chuo
hicho chini ya ulinzi wa Polisi, kiongozi huyo alisema huduma ya maji
nayo ni kero kubwa chuoni hapo.
“Wakati mwingine zinaweza kupita zaidi ya siku mbili
hatujaoga; yote hayo ni kwasababu tuaambiwa na uongozi wa chuo kwamba
hawana fedha za kulipia huduma hizo,” alisema.
Makamu Mkuu wa Chuo hicho, Anjelist Mlenga alisema
uongozi wa chuo unawaonea huruma wanafunzi hao lakini akakosoa taratibu
wanazozitumia kudai huduma hizo.
Akiwa hajui kiasi cha fedha kinachodaiwa kwa ajili ya
huduma ya maji, Mlenga alisema deni la umeme chuoni hapo ni zaidi ya Sh
Milioni 2.5.
Alisema Mkuu wa chuo hicho amekwenda wizarani kufuatilia fedha hizo kwakuwa wao ndio wenye jukumu la kulipia huduma hizo.
“Mkuu wa Chuo yupo wizarani, naomba muwe wavumilivu
kwani hata kama atakubaliwa fedha hizo, kwa taratibu za serikali inaweza
kuchukua wiki nyingine kuzipata,” alisema.
Akizungumzia ombi la wanafunzi hao la kukifunga chuo
hicho mpaka pale huduma hizo zitakaporejea, Mlenga alisema “ ni jambo
linalojadirika, tutaona mpaka wiki ijayo hali itakavyokuwa na
tutaangalia cha kufanya.”
Aliwasihi wanafunzi hao kuacha kuyachanga madai yao na
itikadi zao za kisiasa kwa kuzingatia kwamba mambo hayo yanapigwa
marufuku katika taasisi za elimu.
Wanafunzi hao wakiwa na mabango mbali mbali leo katika viwanja vya chuo hicho
Polisi wakithibiti maandamano hayo
WAnafunzi hao wakiwa katika viwanja vya chuo hicho leo
Makamu Mkuu wa Chuo, Mlenge |
Rais wa serikali ya wanafunzi, Manfred Joachim |
0 comments:
Post a Comment