Hali hii ilipomuanza, alianza kwa kulia machozi mekundu, kutokwa na damu puani na kunyunyukwa nywele kichwani.
Hali ilipokuwa mbaya, alikuwa akienda hedhi kwa siku 15
mpaka ikafika kipindi alihitaji kuongezwa damu kutokana na hali hiyo
iliyokuwa ngumu. Licha ya vipmo vingi alivyofanya, madaktari wa mji wake
wa Veron, kwenye Jamhuri ya Dominica, walishindwa kumsaidia.
Cedeno alisema: ‘Hali hii ilipoanza kwangu sikuwa najua nini cha kufikiri – nilishtushwa na kuogopa.
Anasema alijisikia vibaya kutokana na hali aliyokuwa nayo
mpaka ikambidi aondoke nyumbani kwao alipokuwa akiishi na mama yake
aitwaye Mariana, 36.
Aliacha shule huku marafiki zake wengi wakimtenga kutokana
na hali hiyo wakihofu kupata maambukizo au usumbufu kutokana na hali
yake.
‘Nilitengwa, ila Mungu mkubwa. Kwa sasa najisikia poa maana baada ya muda mrefu nimeanza kujisikia vizuri.’
Miezi michache baadae alifanikiwa kupata boyfriend,
Recaris Avila, ambaye alimtembelea hospitali mara baada ya kusikia stori
yake.
Sasa, miaka minne baada yote kuanza, madaktari wa wamefanikiwa kutatua tatizo lake.
0 comments:
Post a Comment