Na Waandishi wetu, Mwananchi
Wakati
kuna joto la vyombo vya habari vya kimataifa kuituhumu Tanzania kuwa
haipambani na ujangili, Rais Jakaya Kikwete amesema Serikali imeubaini
mtandao unaojumuisha watu 40, akiwemo tajiri maarufu mkoani Arusha.- Akihojiwa juzi jioni na Idhaa ya Kiswahili ya BBC, Rais Kikwete alikanusha taarifa zilizotolewa na gazeti la Sunday Mail la Uingereza zilizodai Tanzania haijafanya juhudi za kupambana na ujangili wa meno ya tembo, akisema taarifa hizo ni uzushi na upuuzi mtupu.
Akihojiwa juzi jioni na Idhaa ya Kiswahili ya BBC,
Rais Kikwete alikanusha taarifa zilizotolewa na gazeti la Sunday Mail
la Uingereza zilizodai Tanzania haijafanya juhudi za kupambana na
ujangili wa meno ya tembo, akisema taarifa hizo ni uzushi na upuuzi
mtupu.
“Gazeti hilo limezungumza na nani, ndiyo maana
sitaki kupoteza muda kujadili upuuzi, achana na mambo hayo. Ndiyo maana
tunasema, akutukanaye hakuchagulii tusi,” alisema Rais Kikwete.
Alisema inashangaza kuona watu wanaozusha taarifa
hizo hawaoni jinsi tulivyofanya jitihada za kutokomeza ujangili, kama
operesheni za tokomeza ujangili na operesheni kipepeo.
Kuhusu majangili 40 ambao wametambuliwa, Rais
Kikwete alisema wameutambua mtandao mkubwa wa majangili unaoongozwa na
mfanyabiashara mkubwa wa Arusha Mjini.
“Kuna majangili 40 waliotambuliwa na tumetambua
mtandao mzima, pale Arusha kuna mtu mkubwa alikuwa anaendesha biashara.
Kazi ilikuwa ni kutambua mtandano wote, ule mtandao ni mpana sana,”
alisema Rais Kikwete.
Katika mahojiano hayo, Rais Kikwete alisema,
Tanzania ilikuwa ni nchi yenye tembo wengi zaidi duniani, lakini
ujangili ulipokithiri, tembo walipungua na kufikia 57,000 tu mwaka 1987.
“Mwaka 1989, Taasisi ya Kimataifa ya Cites,
walipiga marufuku biashara ya meno ya tembo duniani na ujangili
ulipungua kwa kiasi kikubwa hivyo tembo waliongezeka na kufikia, 110,000
mwaka 2009,” alisema.
Kikwete ahojiwa CNN
Rais Jakaya Kikwete amekiri kuwa vita dhidi ya ujangili ni tatizo sugu linaloielemea Tanzania.
Wakati idadi ya tembo ikiendelea kupukutika kila
siku, vita dhidi ya ujangili ilichukua sura mpya mwishoni mwa mwaka jana
baada ya operesheni iliyofahamika kwa jila la Tokomeza Ujangili,
kukumbwa na kashfa ya ukiukwaji wa haki za binadamu na kusababisha
mawaziri wanne kujiuzulu.
Mawaziri waliojiuzulu ni pamoja na aliyekuwa
Waziri wa Maliasili na Utalii, Balozi Khamis Kagasheki, aliyekuwa Waziri
wa Mambo ya Ndani ya Nchi, Dk Emmanuel Nchimbi, aliyekuwa Waziri wa
Ulinzi na Jeshi la Kujenga Taifa, Shamsi Vuai Nahodha na aliyekuwa
Waziri wa Mifugo na Uvuvi, Dk David
0 comments:
Post a Comment