Sunday, 16 February 2014

MSANII ‘MIRIAM ROBERT’ ADAIWA KUKIMBIA KWAO, SASA ANAISHI NA MUME WA MTU



WAKATI taarifa za juu juu kuhusu msanii wa filamu bongo Miriam Robert, aliyekimbia kwao zikileta utata wapi alipo, mwandishi wetu amenasa taarifa hizo ambapo inadaiwa kuwa msanii huyo ameolewa na ndoa hiyo haitambuliki na ndugu yeyote hivyo baadhi ya ndugu na rafiki wanaamini kuwa atakuwa anaishi na mume wa mtu.


Taarifa za awali ambazo zilifika mezani mwa mtandao huu zilidai kuwa awali msanii huyo alikuwa akiishi kwao lakini alikuja kuondoka kwa utata bila mtu yeyote kujua, huku akiwapa wakati mgumu wazazi wake ambao hadi walifikia hatua ya kutaka kutoa taarifa polisi.



Baada ya mtandao huu kufanya uchunguzi kwa kuzungumza na baadhi ya rafiki zake wa karibu, ambapo hata hivyo hawakutaka majina yao yatajwe walidai, Miriam anaishi hapa hapa Dar na yupo na mume wa mtu.



Rafiki hao walidai kuwa hata hivyo kitendo cha kuishi na mume wa mtu kinaweza kumletea madhara makubwa na waliomba ni bora arudi nyumbani ili aweze kuwatuliza wazazi ambao hadi sasa bado hawana mawasiliano naye.



“Sisi ni rafiki zake na hatuna habari kwamba ameolewa bali tunavyojua ni kwamba lazima atakuwa anaishi na mtu, kama ndoa ingejulikana mbona wazazi wake hawajui kama kaolewa tena alipotoka kwao hakuna mtu aliyejua, anaishi na mume wa mtu,” walisema.


Hata hivyo mwandishi wa habari hizi, alipojaribu kupiga simu yake ilipatikana, na alipoulizwa juu ya ishu hiyo alidai kuwa ni kweli ameolewa na anaishi na mtu na suala la watu kudai wamechukuana kimya kimya haliwahusu.



“Naishi mume wangu kwani hao wanaosema nimetoroka nyumbani inawahusu nini nafanya kile roho yangu inataka wao nao wana maisha yao kwanza hata wao wanatembea na waume za watu mbona hatusemi,” alidai Miriam.

0 comments:

Post a Comment