MSANII wa kike katika filamu za Kibongo, Wastara Juma amewashukia watu wanaotafsiri kila kitu anachokifanya katika maisha yake na kusema: “Yaani nisipige picha nikaweka kwenye mitandao ya kijamii, tayari watu wanasema yao...jamani nami pia ni binadamu.”
Wastara ambaye ni mjane wa marehemu Juma Kilowoko ‘Sajuki’ ameliambia gazeti hili wikiendi iliyopita kuwa, baada ya kuachwa mpweke na mumewe Sajuki, watu wanafuatilia sana maisha yake kiasi kwamba anakosa uhuru.
Alisema, wengine hutafsiri vibaya hata wanaume anaokuwa nao karibu kikazi au marafiki, akafafanua: “Nashangaa kila nitakachofanya kinaanikwa na kuonekana ni kibaya wakati nami ni binadamu ninao uhuru wa kufurahi na kujiachia nitakavyo ili mradi sijavunja maadili.”
0 comments:
Post a Comment