Wednesday, 6 November 2013

SERIKALI YAKUTANA NA UJUMBE WA SYMBION KUJADILI UJENZI WA KITUO CHA SOKA (SOCCER ACADEMY)




Katibu Mkuu Wizara ya Habari, Vijana, Utamaduni na Michezo, Bi. Sihaba Nkinga, akisisitiza jambo, leo Novemba 5, 2013, jijini Dar-es-salaam, alipokutana na ujumbe wa kampuni ya Symbion ya Marekani kujadili maandalizi ya ujenzi wa  kituo kikubwa cha maendeleo ya mchezo wa soka nchini (Soccer Academy), ambayo itashirikiana na Club ya Sunderland ya Uingereza katika kuindesha Academy hiyo. Katika mpango  huo, Kampuni ya Symbion pia itajenga viwanja vya michezo (sports courts) eneo la Kidongo Chekundu. Mazungumzo hayo yamehusisha pia ujumbe wa viongozi kutoka Idara ya Michezo (hawapo pichani)



Mtendaji Mkuu wa Kampuni ya Symbion, Ndugu. Peter Gathercole (kulia) akifafanua jambo, leo Novemba 5, 2013, jijini Dar-es-salaam, alipokutana na Uongozi wa Wizara ya Habari, Vijana, Utamaduni na Michezo kuelezea mikakati ya Maandalizi ya ujenzi wa Kituo cha Maendeleo ya Mchezo wa soka nchini (Soccer Academy), pamoja na viwanja vya michezo (sports courts). Kulia kwake ni wajumbe alioongozana nao.

Mkurugenzi wa Idara ya Maendeleo ya Michezo wa Wizara ya Habari, Vijana, Utamaduni na Michezo, Ndugu. Leonard Thadeo (kushoto) akielezea jambo, leo Novemba 5, 2013, jijini Dar-es-salaam, wakati uongozi wa Wizara ulipokutana na Ujumbe wa Viongozi wa kampuni ya  Symbion ya Marekani Kujadili Maandalizi ya Ujenzi wa Kituo Kikubwa cha Mchezo wa soka nchini (Soccer Academy), pamoja na viwanja vya michezo (sports courts). Kulia kwake ni Katibu Mkuu wa Baraza la Michezo la Tanzania (BMT), Henry Lihaya  na Afisa Michezo Mkuu, Charles Yasse Mattoke

Viongozi wa Wizara ya Habari, Vijana, Utamaduni na Michezo wakiwa katika mazungumzo na Ujumbe wa Viongozi wa  Kampuni ya Symbion ya Marekani walipokutana, leo Novemba 5, 2013, jijini Dar-es-salaam kujadili maandalizi ya ujenzi wa Kituo cha Maendeleo ya Mchezo wa soka nchini (Soccer Academy), pamoja na viwanja vya michezo (sports courts).

0 comments:

Post a Comment