Hata kama sio shabiki wa diamond ila kuna kitu lazima uwe kinakuvutia kutoka kwake.Unaweza kujitahidi kumchukia labda kutokana na skendo zake za nje ya muziki wake ila ukirudi kwenye muziki wake nadhani anastahili kuwa pale alipo.

Kuanzia muonekane wake mpaka anavyoweza kuji-brand kimataifa na anavyojua kucheza na akili za mashabiki.
Wasanii wengi wa bongo flava wana tabia ya kurithika kwa mafanikio yao ila Diamond toka atoke na Kamwambie mwaka 2009 mpaka 2013 amezidi kwenda juu bila kuonyesha kusuasua wala kutetereka.
Angalia video ya number 1.Wimbo unaweza sema ni wa kawaida kabisa ukilinganisha na mbagala, kamwambie au nitarejea ila akili ya kwenda kufanya video cape town,south africa kumeifanya nyimbo iwe number 1 kama jina lake lilivyo.

Ushawahi kujiuliza Ali kiba yupo wapi pamoja na kuwa kila mtu anajua ni mkali kuliko diamond?Ali kiba toka atoe my everything mwisho wa mwaka jana amepotea hata video ajatoa.Tukaja kumuona kwenye kidela na Abdu kiba bila kurefusha maneno Ali anashindwa kuufanya mziki wake kama mashabiki wake wanavyotarajia labda pengine angekuwa anafukuzana na diamond ila matokeo yake vijana wake kama Rich mavoko na Dimpoz ndio wapo nyuma ya Diamond huku Ali akibaki msanii mkali ambae ameshindwa kuendelea kutuonyesha ukali wake sijui anawaza nini!