Saturday, 22 February 2014

KWA NINI WANAUME WENGI SIKU HIZI HAWAPENDI KUOA...?? SOMA HAPA KUJUA SABABU..


Kumekuwa na maswali yasiyo na majibu miongoni mwa jamii kwamba imekuaje vijana wa kiume wamekuwa ni waongo sana hasa linapokuja swala la kuoa? Kwa kadiri siku zinavyozidi kwenda ndivyo ambavyo idadi ya wanaume wanaoogopa kuoa inazidi kuongezeka. Utakuta wapenzi wanaambiana kwamba wanapendana na kuahidiana kuwa wataoana, lakini kitakachotokea baada ya hapo ni mwanaume kuanza kupiga chenga kwa visingizio lukuki.

Kwa nini hali hiyo hutokea?

Ukweli ni kwamba hakuna jibu la moja kwa moja juu ya tatizo hilo, lakini yapo mambo ambayo yanaweza kutupa angalau tafakuri. Nitajaribu kudadavua baadhi ya sababu zinazowafanya wanaume siku hizi kukwepa kuingia katika taasisi ya ndoa:

1 Ukosefu wa mtu wa kumchukulia kama mfano:
Hapa nawazungumzia wale watoto wa kiume waliolelewa malezi ya upande mmoja yaani walilelewa na mama peke yao. Sina maana ya kudharau au kutweza malezi ya mama, la hasha, lakini ni vyema mkafahamu kwamba kuwa na baba asiye na malezi mazuri si sawa na kutokuwa na baba. Na ndio maana nikasema ukosefu wa mtu wa kumchukulia kama mfano. Achilia mbali aina ya malezi atakayoyapata kwa familia yawe mazuri au mabaya lakini lazima kutakuwa na tabia za kiume zitakazoakisi malezi ya mtoto wa kiume katika familia husika. Watoto waliolelewa na mama peke yao kuna kitu huwa wanakosa, kwani wanakuwa hawana mtu wa kumchukulia kama mfano kwa upande wa jinsia ya kiume na hapo ndipo hujikuta wakijifunza wenyewe namna ya kuongea na kutenda kama wanaume kwa sababu katika makuzi yao hawakupata fursa ya kuwa karibu na baba zao. Kwa kuwa siku hizi kuna kundi kubwa la kina mama ambao wamejikuta wakiachiwa mzigo wa malezi ya watoto, baada ya aidha kuachwa na waume zao au kuzalishwa na kutelekezwa (Single mothers), na hapo ndipo tunaposhuhudia mtoto wa kiume anapokua kwa umri na kimo huku akiwa hana mtu wa kumuangalia kama mfano wa mume anavyotakiwa kuwa katika familia zaidi ya kujifunza mambo hayo kupitia katika TV, senema au miziki. Wanaume waliopitia malezi ya aina hii huchelewa sana kuoa kwani huyaangalia maisha ya ndoa kwa namna ya kujaribu na ndipo hapo wengi huishia kuishi kinyumba na wanawake kwa ajili ya kutaka kujifunza namna ya maisha ya ndoa yanavyotakiwa kuwa na ndio sababu huchukua muda mrefu kufanya maamuzi. Na mara nyingi huishia kubadilisha wanawake kutokana na kutokuwa na uhakika wa kile wanachokitafuta.

2 Mgogoro wa kiuchumi:
Kuna kundi kubwa la vijana siku hizi hawana ajira au hawana uhakika na kipato. Ukweli ni kwamba hakuna mwanaume atakayependa kujiingiza kwenye ndoa wakati hana kazi au hana uhakika na kipato chake. Na hiyo ni kutokana na wanawake wengi siku hizi kuonekana kujali zaidi wanaume wenye uhakika na kipato. Hii misemo ya wanawake ya kebehi dhidi ya wanaume wasio na ajira au kipato, kama vile “mwanaume suruale” ina mchango mkubwa sana katika kuwafanya wanaume kukwepa kuoa iwapo hawana ajira au hawana uhakika na kipato chao.


3 Wanawake wengi kuwa na kiwango cha elimu ya juu:
Siku hizi wanawake wengi wameibuka katika kutafuta elimu ya juu kwa juhudi kubwa. Idadi ya wanawake wanaojiunga na vyuo vikuu ni wengi tofauti na ilivyokuwa zamani. Na hiyo ni kutokana na wazazi wengi kubadili mtazamo wao juu ya mtoto wa kike. Zamani mtoto wa kike alichukuliwa kama kitega uchumi. Kwa maeneo ya vijijini na katika familia masikini, watoto wa kike walikuwa wanatazamwa kama, ‘biashara ya kesho’ ambapo watauzwa kwa njia ya mahari. Kwa hiyo thamani yao ilikuwa ni kuolewa, ni ile ya kibidhaa na sio kibinadamu. Lakini tofauti na zamani siku hizi hata kule vijijini kumekuwa na mwamko mkubwa sana wa kumsomesha mtoto wa kike hadi elimu ya juu. Kutokana na mwamko huo wanawake wengi wamejikuta wakiona elimu kama kimbilio pekee la kuepukana na mfumo dume. Mwanamke gani atakubali kunyanyaswa na mwanaume akiwa na elimu yake na labda pia akiwa na kazi yake yenye mshahara na marupurupu ya kutosha, naamini watakuwa ni wachache sana ambao hawajiamini au waliathiriwa na malezi. Kwa upande wa wanaume nao, wamejikuta wakiwaogopa wanawake hawa wenye elimu ya juu kwa hofu ya kuzidiwa kipato na labda kukosa sauti kama mwanaume na hiyo inatokana na ego tu.

4 Wanaume huwaona wanawake kama tishio wanapokuwa na mafanikio makubwa kifedha:
Inaweza kutokea mwanaume anaweza kuwa na uhusiano na mwanamke ambaye labda tu nisema ni mbangaizaji. Wakati huo anaweza kuahidi kufunga ndoa na mwanamke huyo, lakini iwapo itatokea mwanamke huyo akapata mafanikio kibiashara na kuinuka kifedha. Kama mwanamke asipokuwa makini anaweza kusababisha mwanaume huyo akaingia mitini. Sababu kubwa hapo inaweza kuwa ni hofu ya kuogopa kuongozwa na mwanamke. Kumbuka kwamba mfumo dume bado umetawala vichwani mwa wanaume wengi kutokana na malezi. Mwanaume asiyejiamini ni vigumu sana kwake kuoa mwanamke aliyemzidi kipato. Kwa sababu akifanyiwa jambo dogo tu, inakuwa kama ametoneshwa. Atahisi kutaka kutawaliwa na mwanamke huyo. Jambo ambalo wanawake wanatakiwa kulifahamu ni kwamba kila mwanaume anataka kutambuliwa na kuheshimiwa kama shujaa kabla ya kumfuata msichana. Iwapo utakuwa umesimama iwe ni kifedha au kielimu pale unapotafuta kupata mwenza, inabidi ujishushe sana la sivyo utadoda.


5 Wanaume wengi siku hizi wana hofu ya majukumu, hasa ya kulea watoto:
Kutokana na malezi yao au kile wanachokijua kuhusu watoto, baadhi ya vijana huamini kwamba, kulea watoto ni jambo gumu sana. Lakini wengine wanaamini kwamba, hata mke anapaswa kulelewa kama ilivyo kwa mtoto. Hivyo wanaamua kutafuta kwanza uwezo ambao haupatikani kiurahisi. Kuna wengine, ambao wamefundishwa au kuelekezwa na mila na desturi zao kwamba, kabla hawajaoa, ni lazima wawe na nyumba kwanza, tena kwao. Kwa hiyo, hawa hadi waje wapate uwezo wa fedha wanakuwa wameshachelewa.

6 Kuna baadhi ya wanaume, maisha bila ya ndoa wanayaona kuwa ndiyo bora kuliko yale ya ndoa:
Kuna baadhi ya wanawake hujirahisisha sana kwa wanaume. Siku hizi ni jambo la kawaida sana kukuta mwanaume anaishi na mwanamke bila ndoa, wenyewe wanaita Trial Marriage. Na hapo ndipo unapokuta wanaume hawaoni tena umuhimu wa kuoa. Sasa kama mwanamke anaweza tu kuishi na mwanaume bila ya ndoa na mwanaume huyo akapata huduma zote kutoka kwa mwanamke huyo, unadhani ni kitu gani kitamvuta kufunga ndoa. Jambo lingine ni ile dhana kwamba maana ya ndoa ni tendo la ndoa. Siku hizi wanaume wengi wamejikuta wakiwa hawahitaji tena kuoa kwa sababu tendo hilo linapatikana kiurahisi tofauti na zamani. Siku hizi inawezekana kabisa kumtongoza binti leo na kupata tendo siku hiyo hiyo….. Na hapa siwazungumzii makahaba. Nawazungumzia mabinti zetu ambao wengine ukiwaona ni watu wa kuheshimiwa ukiwaangalia kwa nje lakini kwa ndani hawana lolote, vijana wa siku hizi wenyewe huwaita maharage ya Mbeya.

Kuna sababu nyingi zinazotajwa kusababisha wanaume siku hizi kujivuta sana katika kufanya maamuzi ya kutafuta mwenza. Lakini hizo chache nilizozitaja zina mchango mkubwa.

NENO MOJA LATOSHA KUVUNJA NDOA...!! SOMA HAPA..


Kubishana sawa, lakini tuchunge kauli zetu!

Wote sisi, kama binadamu huwa tunashikwa na hasira kutoka muda fulani hadi mwingine, lakini kushikwa na hasira na kuziacha hasira hizo ziwaumize wale tunaodai kuwa tunawapenda ni jambo tofauti sana.

Tunapojikuta tunashindwa kuzuia kulipukwa na hasira dhidi ya wale tunaowapenda mara kwa mara, inapasa tujue pia kwamba tunaujeruhi uhusiano wetu na baadae tutauuwa kabisa.

Kuna wakati kwa sababu mbalimbali, baadhi yetu huwa tunajikuta tukitaka tu kuwakera wapenzi wetu kwa kuwapandishia kila wakati kwa milipuko ya hasira. Ni kama vile, bila kulipukwa na hasira hizo, maisha yetu yanakuwa yamepoteza maana.

Ni vigumu sana wakati mwingine kwa watu hawa kuacha tabia yao hiyo, lakini juhudi ya kujitoa ni muhimu sana. Ni muhimu sana kwa sababu, uhusiano mwingi umevunjika kutokana na hasira hizi za kila wakati, ambazo wala hazina msingi, bali zinatokana na mtu kujichukia mwenyewe.

Kutokana na hasira hizi, mara nyingi wapenzi hujikuta wakilazimika kubishana badala ya kujadili. Hawa watu wenye hasira hizi za hapa na pale, huwa siyo wasikilizaji, bali ni watu wa kulaumu, kujitetea, na kutaka kusikilizwa wao tu, kwa maana ya kushinda.

Katika uhusiano wa aina hii, hakuna uwezekano wa ustawi, bali uwezekano ni uhusiano kufa. Kwani ni mara chache ambapo huyu mpenzi mwenye hasira za mlipuko atakuwa tayari kusikiliza na kuelewa.

Jambo ambalo wapenzi wanapaswa kulifanya,. Bila kujali kama wana hasira sana au hasira nyingi, ni kujitahidi kuweka nguvu kwenye jambo wanalojadili. Watu wenye hasira za ziada, huwa hawana uwezo wa kuzingatia kile kinachojadiliwa.

Huwa na ugumu huo kwa sababu hasira za ziada huwasukuma kusema chochote ambacho kitawafanya washinde, ikiwemo kusingizia na kusema uongo. Lakini huwa wanabebwa na wimbi la hasira kiasi kwamba hawana muda wa kupima athari ya kile wanachosema.

Kuna haja ya kujua kwamba, neno moja tu la hasira, linatosha kuvunja uhusiano au ndoa. Kwa hiyo, ni muhimu sana kwa mtu mwenye hasira za mlipuko kujifunza kuzingatia jambo ambalo, yeye na mpenzi wake wanalijadili. Anapotoka nje ya mada, ni lazima ataropoka.

Kuna wanandoa wanabishana kuhusu shule ya mtoto kwa mfano, mwanandoa mwingine hana haja ya kusema, ‘unabisha kwa sababu hukusoma, ndilo tatizo la kuoa wanawake wasiosoma.’ Hapa ni kutoka nje ya mada kwa hasira za mlipuko.

Kumbuka pia kwamba, wanandoa au wapenzi ambao wanapobishana hawatoki nje ya kile wanachobishania na pia wanatumia nguvu ya hoja badala ya mihemko, huwa wanaelewana katika mambo mengi sana, huwa wanatatua migogoro mingi kwa amani na kuaminiana zaidi.

Kuna wakati kwa sababu ya hasira za mlipuko, mpenzi anaweza kutafuta kwa makusudi jambo ambalo litamuudhi mpenzi wake. Anaweza kumwambia, ‘sibishani na mwanamke mnene kama nguruwe.’ Au mwanamke akamwambia mpenzi au mumewe, ‘mbele ya wanaume nawe unajiita mwanaume.’

Kila mmoja wetu anajua ni maneno gani akisema yatamkera mwenzake. Nasema kila mpenzi anajua eneo nyeti la mpenzi wake, ambalo akiligusa anakuwa amemuuwa kisaikolojia. Kujua huku eneo hilo hakupaswi kutumiwa vibaya na wapenzi.

Kwenye uhusiano kuna kanuni ya, ‘usimtendee mwenzio yale ambayo hupendi kutendewa.’Wapenzi wanapoweza kila mmoja kufuata kanuni hii, uhusiano huwa mzuri sana.

Kuna wakati mpenzi anaweza kudhani kwamba wakati wa kubishana ndio wakati mzuri kwake ‘kumpasha’ mpenzi wake, ndiyo wakati mzuri wa kumuumiza kihisia. Hili ni kosa la karne kwa sababu wakati huu, ndio ambao mwanandoa au mpenzi anapopaswa kujilinda na kauli zake kuliko waati mwingine.

Maneno ndio silaha kwenye kubishana kumbuka. Kwa hiyo yanatumika vizuri au vibaya ni jambo la msingi sana. Maneno huumiza na kuvunja mifupa kuliko vyuma, anavyoweza kupigwa navyo mtu.

Mtu anapojifunza kubishana bila kutumia maneno ya kuumiza au kutoka nje ya mada inayojadiliwa, hujenga kujiamini, kwani mara nyingie hasira za ziada ni matokeo ya kutojiamini.

Inaonekana kuna aina ya maradhi ya kisaikolojia, ambapo mtu hujikuta hawezi kuishi maisha ya amani na mpenzi.

Akihisi amani ni kubwa, hutafuta njia ya kuiondoa ili ajisikie vizuri. Kwa hiyo, atazua jambo ambalo litazua ubishi ambao utamfanya aropoke.

DIAMOND KUHUDHURIA TUZO ZA 'AFRIMMA' ZITAKAZOFANYIKA TEXAS MAREKANI, ZITAHUSISHA WASANII WAKUBWA AFRIKA..



July 26 mwaka huu, wasanii wengi wakubwa Afrika kutoka katika mataifa ya 17 watakutana Dallas, Texas, Marekani kuhudhuria utoaji wa tuzo za kiafrika zinazojulikana kama ‘AFRIMMA Awards’, na tayari Diamond Platinumz tayari ameshaonesha uthibitisho wa kuwa katika daftari la mahudhurio siku hiyo.
 
Diamond amepost kwenye Instagram video inayomuonesha akifanya promo maalum iliyoandaliwa na watayarishaji akiwaambia mashabiki kwa swag za kimarekani kuwa atakuwepo siku hiyo, na kisha akaisindikiza na maneno yanayosomeka, “Yess! i'll be ryt there....Afrimma Awards 26/07/2014 Texas, Dallas (USA).”
 
Tuzo hizo zilizoandaliwa na Big A Entertainment na African Muzik Magazine, zimelenga katika kuwatunuku wasanii mbalimbali wakubwa wa Afrika waliopo duniani kote na itagusa nyanja mbalimbali za burudani ikiwa ni pamoja na wasanii wa muziki, wachezea santuri aka Dj’s, watayarishaji wa muziki, mameneja na watu wanaousapoti utamaduni wa Afrika.
 
Tuzo hizo zinatarajiwa kusindikizwa na vicheko vya mara kwa mara kwa kuwa mshereheshaji wa shughuli hiyo ni mchekeshaji maarufu wa kimataifa, The Basket Mouth na atakuwa na muigizaji mrembo wa Nollywood, Juliet Ibrahim.

JE UNAZIJUA MBINU ZA KUMUACHA MKE MKOROFI....?? SOMA HAPA KUJUA..



Kuna wanaume ambao wametokea kuoa wanawake ambao wana tabia mbaya . ninaposema kuwa na tabia mbaya sina maana ya mwanamke kuwa Malaya, maana hiyo ni fasili rahisi ya tabia mbaya kwa watu walio wengi. Ninaposema tabia mbaya nina maana kwenda kinyume na matarajio ya mume na pengine hata kwenda kinyume na matarajio ya jamii. Mwanamke ambaye ana tabia kama ghubu, mdomo mdomo (mkosoaji), mtapanyaji wa mali, mpenda makuu na tabia nyingine za aina hiyo, ni mwanamke ambaye kwa kiasi kikubwa anaweza kumsababishia mume matatizo ya kimwili na kisaikolojia. Mwanamke wa aina hii anaweza hata kuathiri makuzi ya watoto na kuathiri uhusiano na mume na watu wengine waliyo karibu yake. Kama mwanamke wa aina hii ameolewa na mume mweledi ndoa inaweza isiyumbe sana, lakini hii ina mipaka na kiwango chake.

Kuna wakati matatizo haya huweza kufika mbali zaidi kiasi kwamba huanza kumwathiri mume. Mwanaume ambaye huchukua kila uamuzi unaohusu maisha yake kwa hadhari kubwa, anaweza kuendelea kuishi na mke huyu. Lakini mara nyingi kuendelea kuishi na mke huyu kuna maana ya matatizo zaidi kuliko ufumbuzi. Bila shaka mmeshawahi kusikia wanaume ambao wanalalamika kuhusu tabia mbaya za wake zao (hata hapa JF wapo wengi sana), lakini huku wakiendelea bado kuwa na wake hao. Ukiacha sababu ya kugawana mali, wanaume wengi huwa wanafikiria mambo mengi ambayo huwazuia kuchukua uamuzi wa kuachana na wake hao.

Nimeona itakuwa vizuri kuwaambia wanaume hawa kwamba, kama ndoa zao zimefikia mahali ambapo zinataka kuwatia kichaa, wakiwa na uhakika kwamba wake zao ndio wenye matatizo na sio wao, (hili inabidi waliangalie kwa makini) inabidi wafanye uamuzi kwa kujiangalia wao na watoto wao zaidi kuliko watu au vitu vingine. Baadhi ya mambo ya kuangalia ni haya:

1. Kuathirika kwao: wajiulize wanaumia kiasi gani kimwili na kisaikolojia kwa kuendelea kuishi kwao na wanwake hawa. Kama ni ghubu na kukosolewa, kunawaathiri kiasi gani,? Na kama ni utumiaji mbaya wa mali unawaathiri kwa kiasi gani? Kama athari za tabia mbaya alizo nazo mwanamke zinafaa kudharauliwa na mume anaweza kuzidharau ni vyema akafanya hivyo, na kuendelea na maisha. Na kama akiona kuzidharau tabia hizo itakuwa na maana ya angamio kwake na pengine mbaya zaidi kwa watoto, inabidi hiyo iwe ni sababu ya msingi kuachana na mke huyo.

2. Ndugu watasemaje: wanaume wengi hukwamia hapo. Kama wake zao wanaelewana vizuri na baadhi ya ndugu, au hata wazazi wao, wanaume hushindwa kutoa maamuzi wa kuwaacha kwa hofu ya kulaumiwa na kushangawa. Wakati mwingine mume huyu anaelewena sana na watu wa upande wa pili, yaani ndugu wa mke na hasa wazazi na pengine wote. Hiki nacho ni kikwazo kikbwa sana, kwani mume hufikiria jinsi atakavyoonekana kwa watu hawa, pale atakapoamua kuchukua uamuzi wa kumuacha mkewe.

3. Sifa moja nzuri: pamoja na kuwa na matatizo, kila binadamu anaweza kuwa na upande mzuri. Kama mwanamke huyu ana sifa fulani ambayo ni nzuri sana, tuseme ni mpishi hodari sana na mkarinu kwa wageni , au labda ni mwaminifu sana katika ndoa, mwanaume anaweza kukwama kutoa uamuzi kwa kudhani au kujidanganya kwamba huenda anaweza asipate mwanamke mwingine mwenye sifa kama hizo. Huku ni kujidanganya kwa sababu kila sifa aliyo nayo binadamu fulani, ya kitabia, ipo kwa binadamu mwingine hata kama siyo wengi.

Ukweli ni kwamba mwanaume anaweza kushindwa kumpa talaka mkewe ambaye anakaribia kumuuwa kwa matatizo yake kwa sababu ambazo mtu mwingine anaweza kuzishangaa. Lakini jambo la msingi kwa mwanaume kama huyu ni kujaribu kupima kwa makini, je hizo sababu zinazomfanya asite kuachana na mkewe huyu zina nguvu au maana kuliko maisha yake, hasa mwili na akili yake?.

Angalizo: Sishauri watu kuachana, lakini nashauri watu kujua kwamba ndoa zenye mashaka makubwa ni hatari kwa afya na maisha yao.

FUMANIZI..!! MUME AFUMANIWA NA MWANAMKE MWINGINE CHUMBANI ,,,,,,,,,,,,,,,,,,,

Fumanizi la aina yake lilitokea juzikati asubuhi ya saa 2, Mtaa wa Mbwela, Tandika jijini Dar ambapo mjamzito aliyejulikana kwa jina la Semeni  alipata ‘kichaa’ cha muda baada ya kumfumania mumewe, Dullah akiwa na mwanamke  mwingine chumbani kwao.
Akisimulia mkasa huo, Semeni mwenye ujauzito wa miezi 6 alisema kabla ya tukio aligombana na mumewe akarudi kwao kwa muda wa siku mbili lakini walikuwa wakiwasiliana mpaka asubuhi ya tukio ambapo alimpigia simu kumwambia anafuata nguo kwa vile anakwenda kliniki.
“Nilipokuwa njiani nilimpigia simu mume wangu, nikamwambia nimekaribia, lakini akasema yeye amekwenda Posta.
“Pamoja na majibu hayo, niliamua kwenda. Nilipofika nilikuta mlango umefungwa kwa ndani, nikampigia simu mume wangu, akasisitiza hakuna mtu, yeye yupo Posta.

“Nilichungulia na kuona funguo, nikajua kuna mtu ila hataki kunifungulia, hapo wasiwasi ukazidi kwamba huenda kuna jambo linaloendelea,” alisema Semeni.
Mwanamke huyo aliendelea kuanika kwamba kufuatia hali hiyo aliwaita majirani ambao ilibidi wamtishe mtu aliye ndani kwamba asipofungua watavunja mlango, ndipo mlango ukafunguliwa na kumkuta Dullah akiwa na mwanamke mwingine chumbani, lakini mumewe huyo alichoropoka na kukimbia.
“Nilishtuka, nikapiga kelele ya mshangao kutokana na kitendo alichokifanya mume wangu, kumleta hawara mpaka kwenye chumba tunacholala!
“Sijaamini kilichotokea! Yule ni mume wangu, amewezaje kumleta mwanamke ndani ya chumba tunacholala tena kuna wapangaji wenzangu wameshuhudia,” alisema mwanamke huyo huku akilia machozi.
Akaendelea: “Mimi hapa nyumbani siachiwi hela ya kula, kila siku nakula nyumbani kwetu,  nikijua labda mume wangu hana, kumbe anamalizia kwa hawara! Jamani inaniuma sana, kama hivyo bora amuoe basi tuje tuishi wote au aniache akae yeye.”
Akizungumza na gazeti hili kwa uso ‘uliochunwa’, mwanamke aliyedaiwa kufumaniwa, Mwanaidi huku akiwa ‘ametaitiwa’ ndani, alijitetea kuwa hakufahamu kama Dulla ana mke.
“Mimi aliniambia hana mke wala mtoto na ndiyo maana nilikubali kuanzisha uhusiano wa kimapenzi na yeye si vinginevyo, kama ningejua nisingekubali kuja, kwa hiyo siyo kosa langu,” alisema Mwanaidi.
Baada ya hali kutulia, baba mzazi wa Dullah ambaye anaishi jirani aliitwa kuamua ugomvi huo na kuamuru wote waende nyumbani kwake ambapo  aliagizia gari.
Wawili hao walipofika nyumbani kwa mzazi huyo walimshusha Semeni na kumtaka atangulie ndani, alipoingia tu, nyuma dereva alitakiwa kuondoka gari hilo kwa kasi  huku Mwanaidi akiwemo ndani ili kumnusuru.

Friday, 21 February 2014

Huyu Ndiye Kimwana Anayedaiwa Kuwaambukiza ‘UKIMWI’ Mastaa Nchini Kenya…!!

VANESSA
Kupitia mtandao wa Kenyan Post, hivi karibuni walipost stori ya mwanadada mwenye umri wa miaka 16 ambaye aitwaye vanesa chettle ilidaiwa kuwa ni mwathirika wa ugonjwa wa Ukwimwi na amekuwa akiwaambukiza kwa makusudi mastaa wa nchini humo.Msichana huyo inasemekana ameshafanya mapenzi na watangazaji wa kituo kimoja cha radio ambao ni Shafie Weru na Nick Mutuma, pia ameshafanya mapenzi na mwigizaji Effy, na sasa mwanadada huyo mwenye umri wa miaka 16 anaishi na kibabu cha Kizungu chenye cha umri wa miaka 80, pia inasemekana Vanesa ameshapiga ‘group sex’ na Top Kenya n deejays kwenye pati.
Inasemekana kuwa msichana huyo ni mcheshi na mtundu sana uwanjani, inadaiwa kuwa ameshatembea na waume za watu na mara kibao amekamatwa na polisi lakini huyo babu wa kizungu tajiri anayeishi naye huwa anawapa mitonyo polisi na kumtoa.

ABU KIBA AFUNGUKA SABABU ZA KAKA YAKE "ALI KIBA" KUWA KIMYAA..SOMA HAPA KUZIJUA

 
Ali Kiba, mwimbaji aliyewahi hutajwa na mfalme wa R&B duniani Robert Kelly kama mmoja kati wa wasanii wenye sauti poa zaidi katika mradi wa One 8 amekuwa kimya kwa kipindi cha mwaka mmoja, huku wengi wakitoa sababu kadhaa za kufikirika kuhusu ukimya wake.
Tovuti ya Times Fm imeongea na ndugu wa damu wa Ali Kiba, Abul Kiba ambaye mbali na kuwa msanii aliyetambulishwa kwenye game na kaka yake, amekuwa akisaidia kuzifuatilia na kuzisimamia kazi zake.
Abdu Kiba ameeleza kuwa ukimya wa ndugu yake unatokana na kubanwa na majukumu ya kifamilia.
“Unajua watu wengi wanahisi vibaya sana, mara mwingine anaibuka na kusema amefulia kwenye game,sio kweli naomba niweke sawa kuhusu suala hili ni kwamba Ally Kiba alikuwa na majukumu ya kifamilia pamoja na kazi zake,maana nakumbuka tangu anitambulishe kwenye muziki wa Bongo Flava ndio alianza kubanwa na mambo  yake binafsi.” Amesema Abdu Kiba.
Hata hivyo, mashabiki wa Ali Kiba wana kila sababu ya kukaa mkao wa kusikia hits za mkali huyo mwaka huu.
“Niliwahi kuzungumza nae hivi karibuni, akaniambia mwaka huu anatarajia kuja kivingine katika game. Kwa sasa anajaribu kumalizia baadhi ya nyimbo alizorekodi ili mwaka huu mashabiki wazisikie katika vituo mbalimbali vya radio.” Abdu Kiba aliieleza