
Kumekuwa na maswali yasiyo na majibu miongoni mwa jamii kwamba imekuaje
vijana wa kiume wamekuwa ni waongo sana hasa linapokuja swala la kuoa?
Kwa kadiri siku zinavyozidi kwenda ndivyo ambavyo idadi ya wanaume
wanaoogopa kuoa inazidi kuongezeka. Utakuta wapenzi wanaambiana kwamba
wanapendana na kuahidiana kuwa wataoana, lakini kitakachotokea baada ya
hapo ni mwanaume kuanza kupiga chenga kwa visingizio lukuki.
Kwa nini hali hiyo hutokea?
Ukweli ni kwamba hakuna jibu la moja kwa moja juu...